Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote tupate taufiki ya kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani wao ndio Njia iliyonyooka, na atakayeshikamana nao wao na Qur'an Tukufu, huyo ataepukana na upotevu, kwa sababu wao ndio sehemu ya Kizito cha pili baada ya Qur'an Tukufu, na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ametuusia katika Hadithi Sahih na Mutawatiri ya Thaqalayni, kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na Quran Tukufu ili tuje kupotea baada yake.
Sheikh Mselem: "Mayahudi walikuwepo Madina. Lakini walileta ukorofi na kibri, wakawa wakivunja makubaliano waliyokuwa wakiingia na Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) akawatandika na kuwatimua kutoka katika Bara Arabu">