25 Julai 2025 - 11:33
Imam Sajjad (a.s): Mlinzi wa Ujumbe wa Karbala kwa Dua, Subira na Ukweli – Sheikh Athman Akbar

Sheikh Athman Akbar alihimiza jamii ya Kiislamu kuiga nyayo za Imam Sajjad (a.s) kwa kuitumia dua kama silaha ya kiroho, kuimarisha subira katika majaribu, na kusimamia ukweli mbele ya dhulma ili kuendeleza ujumbe wa Karbala katika zama zote.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika kipindi cha siku tano za mawaidha ya kina, Sheikh Athman Akbar alieleza kwa ufasaha nafasi muhimu na ya kipekee ya Imam Ali ibn al-Husayn Zaynul Aabidin (as), maarufu kama Imam Sajjad, katika kuhifadhi na kuendeleza ujumbe wa Karbala baada ya tukio hilo lenye majonzi makubwa katika historia ya Uislamu.

Imam Sajjad (a.s): Mlinzi wa Ujumbe wa Karbala kwa Dua, Subira na Ukweli – Sheikh Athman Akbar

Sheikh Athman alibainisha kwamba ingawa Imam Sajjad hakushiriki moja kwa moja katika mapambano ya kivita kutokana na maradhi makali aliyoyapata wakati huo, alichukua jukumu kubwa la kimaanawi na kimkakati katika kudumisha ujumbe wa shahidi wa Karbala, Imam Husayn (a.s).

Kwanza, kupitia dua zake za kina, kama vile Du’a Abu Hamza Thumali na Sahifa Sajjadiyya, Imam Sajjad alihifadhi misingi ya tauhidi, haki za binadamu, na maadili ya Kiislamu kwa njia ya kiroho na mafundisho ya ndani ya moyo. Sheikh Athman alieleza kuwa dua hizi zilikuwa chombo cha kisiasa, kijamii na kielimu katika zama za ukandamizaji wa Bani Umayyah.

Imam Sajjad (a.s): Mlinzi wa Ujumbe wa Karbala kwa Dua, Subira na Ukweli – Sheikh Athman Akbar

Pili, alisisitiza umuhimu wa subira ya Imam Sajjad, hasa wakati wa mateka alipokuwa akiongoza wanawake na watoto wa familia ya Mtume (s.a.w.w) kutoka Karbala hadi Sham. Subira yake siyo tu ya kimwili bali ya kiroho na kisiasa, alipojibu kwa hekima dhulma na kejeli za watawala wa zama hizo.

Imam Sajjad (a.s): Mlinzi wa Ujumbe wa Karbala kwa Dua, Subira na Ukweli – Sheikh Athman Akbar

Tatu, kupitia msimamo wake wa ukweli mbele ya madhalimu, hususan hotuba yake ya kihistoria katika jumba la Yazid, Imam Sajjad aliweka wazi uhalisia wa Karbala na kulinda heshima ya Ahlul-Bayt kwa ujasiri mkubwa. Sheikh Athman aliongeza kuwa hotuba hiyo iligeuza mitazamo ya wengi waliodanganywa na propaganda za dola ya Kiumayyah.

Kwa kumalizia, Sheikh Athman Akbar alihimiza jamii ya Kiislamu kuiga nyayo za Imam Sajjad (a.s) kwa kuitumia dua kama silaha ya kiroho, kuimarisha subira katika majaribu, na kusimamia ukweli mbele ya dhulma ili kuendeleza ujumbe wa Karbala katika zama zote.

Imam Sajjad (a.s): Mlinzi wa Ujumbe wa Karbala kwa Dua, Subira na Ukweli – Sheikh Athman Akbar

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha