Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, ameongoza Maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule ya Kilinjiko Islamic Secondary wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi za dini, pamoja na wananchi kutoka maeneo ya jirani.
Katika hotuba yake, Mufti Zubeir alitoa wito kwa Waislamu kote nchini kuhakikisha wanawapatia watoto wao elimu ya dunia sambamba na elimu ya dini. Alisema taifa haliwezi kusonga mbele bila kuwa na wataalamu wa fani mbalimbali kama udaktari, uhandisi, sheria na ualimu.
Alisisitiza kuwa elimu ya dini ni muhimu kwa msingi wa maadili mema, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya elimu ya dunia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa. “Tunapaswa kuwa na masheikh na maimamu, lakini pia tuwe na madaktari, wahandisi na wanasayansi,” alisema.
Chanzo cha Habari: @ibnnews
Your Comment