Mufti
-
Kesi ya Mufti wa Zamani wa Syria Yakabiliwa na Hukumu; Waendesha Mashtaka Wadai Adhabu ya Kifo
Kesi ya Ahmad Badr al-Din Hassoun, Mufti Mkuu wa zamani wa Syria, imeingia hatua ya mwisho baada ya kikao cha tano katika Mahakama ya Jinai ya Nne mjini Damascus. Waendesha mashtaka wamewahi kuomba apewe adhabu ya kifo kwa tuhuma za kuchochea vurugu na kuunga mkono ukandamizaji wa serikali iliyopita, huku tarehe 24 Agosti ikiwekwa kwa ajili ya mapitio ya mwisho na kutolewa kwa hukumu.
-
Ayatullah Arafi asisitiza umoja wa Kiislamu katika barua kwa Mufti Mkuu wa Romania
Ayatullah Alireza Arafi, Mkuu wa Vyuo vya Dini nchini Iran, amesisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja wa ulimwengu wa Kiislamu katika barua aliyompelekea Sheikh Yusuf Murad, Mufti Mkuu wa Waislamu wa Romania. Pia ametangaza utayari wa Vyuo vya Dini vya Iran kushirikiana na Dar al-Ifta ya Romania katika nyanja za kielimu, kitamaduni na utafiti.
-
Baraza la Ulamaa BAKWATA Lamsimamisha Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lateua Kaimu Katika Nafasi Hiyo
Baraza la Ulamaa la BAKWATA, katika kikao chake cha dharura kilichoongozwa na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Khamis Ngeruko, limeazimia kumsimamisha Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam na kumteua Sheikh Abbas Ramadhani kukaimu nafasi hiyo.
-
Mahakama ya Damascus Yaanza Kesi dhidi ya Aliyekuwa Mufti wa Syria, Ahmad Hassoun, kwa Tuhuma za Kuhamasisha Uhalifu wa Kivita
Mahakama ya Jinai ya Nne mjini Damascus imeanza kusikiliza kesi dhidi ya aliyekuwa Mufti wa Jamhuri ya Syria, Ahmad Hassoun, anayekabiliwa na tuhuma za kuchochea mauaji, kuhalalisha uhalifu wa kivita na kutoa uungwaji mkono wa kidini na kisiasa kwa utawala wa zamani wa Bashar al-Asad na washirika wake.
-
Mufti Mkuu wa Tanzania:
"Qur’an Tukufu Inahimiza Amani Kama Msingi wa Maisha ya Mwanadamu | Tunajifunza Amani Kutoka Katika Kisa cha Nabii Ibrahim (as)
Katika kufafanua hoja yake, Mufti Mkuu wa Tanzania ametaja kisa cha wageni wa Nabii Ibrahim (as) kama kinavyosimuliwa ndani ya Qur’an Tukufu. Amesema kuwa wageni hao walipoingia nyumbani kwa Nabii Ibrahim (as), walimpa maamkizi ya amani, naye akajibu kwa maamkizi yale yale ya amani.
-
Mufti Mkuu wa Australia alilaani shambulio la silaha huko Sydney
Mufti Mkuu wa Australia na New Zealand amelilaani vikali shambulio la silaha lililotokea katika Ufukwe wa Bondi, Sydney, na kulitaja kuwa ni kitendo cha kigaidi.
-
Mufti wa Tanzania Atoa Wito wa Kulinda Amani na Kuepuka Uchochezi wa Kidini na Maandamano Yanayopangwa Kufanyika 9 Disemba
"Tuepuke upepo mbaya unaosambazwa kwa chuki za kidini. Sisi Waislamu hatukatazwi kuishi kwa wema na wasiokuwa Waislamu. Maisha ya watu lazima yalindwe,” alisema Mufti.
-
Mufti Mkuu Sheikh Dkt. Abubakar Zubair akutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kujadili kuhusu njia za Kuimarisha Maadili na Ucha Mungu katika Jamii
Ziara hii ya Mufti Mkuu ni miongoni mwa juhudi endelevu za uongozi wa Kiislamu nchini katika kujenga maadili, amani na mshikamano wa kijamii, sambamba na kutoa wito wa kuzingatia uadilifu na uchamungu katika kila nyanja ya maisha.