"Tuepuke upepo mbaya unaosambazwa kwa chuki za kidini. Sisi Waislamu hatukatazwi kuishi kwa wema na wasiokuwa Waislamu. Maisha ya watu lazima yalindwe,” alisema Mufti.
Elimu ya dini ni muhimu kwa msingi wa maadili mema, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya elimu ya dunia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa. “Tunapaswa kuwa na masheikh na maimamu, lakini pia tuwe na madaktari, wahandisi na wanasayansi,”.