Elimu
-
Iran na Siri ya Hasira ya Marekani:
Tatizo la Marekani si Iran Kumiliki Bomu la Nyuklia, bali ni Iran kuwa na Uwezo wa Kujitegemea katika Teknolojia ya Nyuklia
Kibri cha dhalimu huyu (Marekani/Trump) hakimaanishi kwamba Mwenyezi Mungu amempuuza au amemsahau. Kinyume chake, kadiri dhalimu anavyozidi kujipandisha juu kwa kibri na majivuno, ndivyo anguko lake linavyozidi kuwa la kutisha zaidi.
-
Darsa za Kielimu na Maarifa | Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) Yaendelea kuwaangazia Waumini Kila Alhamisi Mjini Moshi +Picha
Kupitia mihadhara hii, waumini hupata fursa ya kujifunza misingi ya itikadi, maadili ya Kiislamu, na mwongozo wa maisha unaojengwa juu ya haki, uadilifu na kumcha Mwenyezi Mungu.
-
Darsa ya Akhlaq kwa Wanafunzi wa Hawza Imam Sadiq (a.s), Kigogo Post – Dar es Salaam, kuhusu: Kibri na Athari Zake kwa Mwanadamu
Kibri ni ugonjwa wa moyo unaoharibu uhusiano wa mwanadamu na Allah, watu, na hata nafsi yake. Kwa mwanafunzi wa Hawza, kibri ni hatari zaidi kwani huua baraka ya elimu na huzuia nuru ya maarifa kuingia moyoni. Njia ya wokovu ni unyenyekevu (tawadhu’), kwani Mwenyezi Mungu huwanyanyua walio wanyenyekevu na kuwashusha wenye kibri.
-
Ni vipi Fatima Zahra (a.s) Alikuwa Mpenzi na Mpendwa Zaidi Katika Maisha ya Ali (a.s)?
Katika baadhi ya nyakati, mtu humtambulisha nafsi yake kwa kutaja nasaba yake na watu wakubwa. Hivyo ndivyo alivyofanya Amirul-Mu'minin Ali (a.s) katika mojawapo ya khutba zake baada ya kurejea kutoka vita vya Nahrawan. Ali (a.s) alisema: “Mimi ni mume wa Bibi Batul, Bibi wa wanawake wa ulimwengu, Fatima aliye mchamungu, msafi, mtukufu, mwongofu, mpendwa wa Mpenzi wa Allah, bora wa mabinti wake na mchanga wa roho ya Mtume wa Allah (s.a.w.).” Kutaja kwa Imam Ali (a.s) daraja la juu la Bibi Zahra (a.s) baada ya kujinasabisha na mwanamke huyu mtukufu ni kusisitiza nafasi kuu ya bibi huyu mbele ya mtu mkubwa kama Ali (a.s).
-
Kenya - Nairobi | Mazungumzo ya Kiutamaduni: Ubalozi wa Iran na APBET SAK Waimarisha Mafungamano ya Kielimu
APBET (Alternative Provision of Basic Education and Training) ni shule za gharama nafuu nchini Kenya zinazolenga watoto wanaoishi katika maeneo yaliyotengwa kama vile mitaa ya mabanda, makazi duni, na maeneo kame au yenye ukame (ASALs).
-
Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Aendelea Kuitangaza Tanzania Katika Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education
Ushiriki wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika majukwaa haya ya kimataifa unaonesha kwa vitendo dhamira yake endelevu ya kuitetea elimu kama nguzo kuu ya maendeleo ya binadamu, sambamba na kuendeleza diplomasia ya elimu kwa manufaa ya mataifa duniani, hususan Afrika.
-
Kikao cha Kamati ya Elimu cha Jamiat Al-Mustafa – Dar es Salaam, Tanzania +Picha
Kikao hiki kimeweka msingi muhimu kwa mustakabali wa elimu na malezi ndani ya Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam-Tanzania, huku wajumbe wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kuboresha mwelekeo wa kielimu na kijamii kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.
-
Ripoti ya ABNA kuhusu Mkutano wa Kitaifa wa Kuheshimika kwa Allama Hassan-Zadeh Amoli:
Elimu, ni amana ya Kimungu ili kuvuka kutoka Ufalme hadi Ufalme wa Mbinguni | Kumheshimu Mwanazuoni, ni wajibu wa kila mtu kwa ajili ya kuingia Peponi
Katika Mkutano wa Kina Kitaifa wa “Mwanazuoni wa Kimungu na Mfuasi wa Tauhidi, Bwana Allama Hassan-Zadeh Amoli” uliofanyika Qom, Ayatollah Hassan Ramadhani, profesa wa vyuo vya kidini, akielezea hadhi ya juu ya elimu kama amani ya Mungu inayohakikisha maisha ya kimwili na kiroho ya binadamu, alisisitiza kwamba elimu halisi inajumuisha maarifa yote ya kuongoza kutoka fiqhi hadi falsafa, na kuheshimu wanazuoni wa kweli ni njia muhimu ya kufikia ukamilifu, kuinua maisha ya kiroho na kuingia Malakut (ufalme wa kiroho).
-
Mwaka mmoja tangu marufuku ya kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq(as); Sera iliyoratibiwa mahsusi kulenga Ibada za Kidini nchin Bahrain
Kwa mujibu wa wachambuzi, kulengwa kwa mimbari ya Sala ya Ijumaa si suala la ndani tu, bali ni ishara ya juhudi za serikali ya Bahrain kudumisha uhusiano wa karibu na Israel - hata kama ni kwa gharama ya kukandamiza sauti za kidini na za wananchi.
-
Ushinikizi wa Taliban kubadilisha Shule za Kidini kuwa njia pekee ya Elimu kwa Wasichana
Mama mmoja mkoani Nimruz alisema baada ya Mullah kumtaka, alilazimika kuwatoa mabinti zake shuleni na kuwapanga kwenye madarasa ya dini, lakini msaada alioahidiwa haukuwahi kufika. Mama mwingine alisema alipewa masharti: “Ama upeleke binti zako kwenye madarasa ya dini, au hupati chochote.”
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s): Uwezo wa Umma wa Kiislamu Unategemea Muunganiko wa Elimu na Imani
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) ameona kuwa muungano kati ya elimu na imani ni wa lazima, na akaeleza kwa kusisitiza kwamba: “Jamii ambayo inamiliki misingi hii miwili kwa pamoja – yaani elimu na imani - hufikia kiwango cha nguvu na mamlaka ambacho hakuna mfumo wowote wa kiutawala au ukoloni unaoweza kupenya ndani yake.”
-
Malawi | Mwanzo Mpya wa Kipindi Kipya: Siku ya Kwanza, Marasimu ya Asubuhi Ikiashiria Matumaini na Mwelekeo wa Mafanikio katika Safari ya Kielimu
Kauli mbiu ya mwanzo mpya ilikuwa: "Elimu ni ufunguo wa mafanikio - tukaze buti tangu mwanzo!"
-
Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Asilimia 92 ya Watu wa Afghanistan Wanataka Elimu kwa Wasichana Kuendelezwa
Wakati Serikali ya Taliban inaendeleza sera za kuzuia elimu kwa wasichana, ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha wazi kuwa watu wa Afghanistan – wanawake kwa wanaume, wa mjini kwa vijijini – wanataka mabadiliko. Wanataka elimu kwa wasichana, fursa za kazi kwa wanawake, na mustakabali bora kwa jamii nzima.
-
Ahadi Mpya za Taliban / Ufunguzi wa Shule za Wasichana Wategemea "Kibali cha Kisharia"
Zabihullah Mujahid, msemaji wa serikali ya Taliban, ametangaza kuwa mchakato wa kupata “kibali sahihi cha kisharia” kwa ajili ya kufunguliwa tena shule na vyuo vikuu vya wasichana bado unaendelea. Hii ni baada ya zaidi ya miaka minne ya kunyimwa wanawake na wasichana haki ya msingi ya elimu.
-
Mmiliki wa Mawkibu Muiraq Katika Mahojiano na ABNA:
Arubaini ni fursa yenye thamani kubwa ya kubainisha uhalisia wa Jamhuri ya Kiislamu na tabia ya kinyama ya Israel
Mmiliki wa Mawkibu kutoka Iraq, akisisitiza umuhimu wa Jihadi ya Kuelimisha katika siku za Arubaini ya Imam Hussein (a.s), amesema kuwa siku hizi ni fursa muhimu ya kuwapa uelewa mataifa mbalimbali.
-
UNICEF: Takriban watoto milioni 4 wa Afghanistan hawana fursa ya kupata elimu
UNICEF imetangaza hivi karibuni kuwa takriban watoto milioni 4 nchini Afghanistan hawapati elimu kutokana na uhaba wa shule, huduma za afya, na walimu wenye sifa.
-
Naibu Waziri wa Elimu na Utamaduni atembelea Shirika la Habari la ABNA / Entemani: Tofauti za ABNA ndizo Nguvu yake
Naibu Waziri wa Elimu na Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran, alipokuwa akitembelea Shirika la Habari la ABNA, alieleza kwamba vyombo hivi vya habari vina sifa za kipekee na vina athari kubwa katika jamii.