Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mubahatha ya kielimu ni nguzo muhimu katika kukuza na kudumisha elimu.
Elimu ya kweli haikamiliki kwa kusoma pekee; bali huimarika zaidi kupitia mijadala ya kielimu, utafiti wa kina, na kubadilishana maarifa baina ya wanafunzi.
Bila Mubahatha, elimu hupungua thamani yake na huweza hata kupotea katika akili ya mwanafunzi au mtu yeyote mwenye maarifa.
Hivyo basi, kusoma lazima kuambatane na Mubahatha na utafiti wa kina ili kuhakikisha elimu inadumu na kunawiri.
Your Comment