Sayansi
-
Jamiat Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salam | Kikao cha Kielimu: Nafasi ya Imam Hassan Askari(as) katika Kuhifadhi Madhehebu ya Shia Kuendeleza Njia ya Uimamu
Katika hotuba yake, aligusia mazingira ya kisiasa ya wakati huo, mbinu za kitaqiyya (kuficha imani kwa sababu za kiusalama), kulea wafuasi maalum, na juhudi za Imam katika kuimarisha misingi ya aqida ya Kishia.
-
Ayatollah Rajabi:
Dhamira kuu ya Taasisi ya Imam Khomeini (rehmatullahi alayh) ni kuzalisha sayansi za binadamu za Kiislamu
Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis Khobregan Rahbari) alisema kuwa Taasisi ya Imam Khomeini (rehmatullahi alayh) ina lengo kuu la kuzingatia nyanja kadhaa muhimu. Aliongeza kuwa taasisi hii inalenga sana masuala ya kielimu, maadili, pamoja na uelewa wa kijamii na kisiasa.
-
Utafiti wa Kielimu – Nguzo ya Elimu ya Kudumu - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salaam - Tanzania
Mubahatha na Utafiti wa Kielimu ni moyo wa Elimu ya Kiislamu. Kupitia mijadala ya kielimu, Wanafunzi hubadilishana maarifa, kufungua milango ya utafiti, na kuimarisha uelewa wa kina wa masomo yao. Ukweli ni kwamba: Elimu bila Mubahatha ni kama mwili bila roho. Hupotea taratibu, na haidumu katika fikra za Mwanafunzi.
-
Wanafunzi wa Hawza ya Imam Ridhwa (as) - Ikwiriri, Tanzania, wakiwa katika makundi yao wakifanya Mubahatha wa kielimu
Bila Mubahatha, elimu hupungua thamani yake na huweza hata kupotea katika akili ya mwanafunzi au mtu yeyote mwenye maarifa.
-
Katika kongamano la Kimataifa la "Sayansi, Dini, na Akili Bandia" lililofanyika Zagreb, Shahriyari:
Akili bandia si dhana bali ni mshirika kwa Binadamu katika kila dakika ya maisha yake
Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Kuleta Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu alisema: Mjadala wa akili bandia ni mpana sana na unahusisha kila nyanja ya maisha ya binadamu, na kila mtu anapaswa kuuhusisha kulingana na wajibu wake mwenyewe.