30 Agosti 2025 - 22:51
Jamiat Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salam | Kikao cha Kielimu: Nafasi ya Imam Hassan Askari(as) katika Kuhifadhi Madhehebu ya Shia Kuendeleza Njia ya Uimamu

Katika hotuba yake, aligusia mazingira ya kisiasa ya wakati huo, mbinu za kitaqiyya (kuficha imani kwa sababu za kiusalama), kulea wafuasi maalum, na juhudi za Imam katika kuimarisha misingi ya aqida ya Kishia.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, tarehe 30 Agosti 2025, kikao maalumu cha kielimu kilifanyika katika Chuo cha Sayansi ya Kidini cha Jamiat Al-Mustafa(s), Jijini Dar -es- Salaam, Tanzania, kwa ushiriki wa wanafunzi na wapenzi Sayansi ya Dini na Historia ya Kiislamu.

Jamiat Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salam | Kikao cha Kielimu: Nafasi ya Imam Hassan Askari(as) katika Kuhifadhi Madhehebu ya Shia Kuendeleza Njia ya Uimamu

Mzungumzaji katika kikao hicho alikuwa: Hujjatul-Islam wal-Muslimin Samahat Sheikh Rayhani Yasin, ambaye alielezea kwa undani nafasi ya kihistoria ya Imam Hassan Askari (a.s) katika kuhifadhi Madhehebu ya Shia Ithna Ashari chini ya mazingira magumu ya kisiasa na kijamii ya zama za utawala wa Bani Abbas, na jinsi alivyoweka msingi wa kuandaa jamii kwa ajili ya Uimamu wa Imam Mahdi (a.t.f.s).

Katika hotuba yake, aligusia mazingira ya kisiasa ya wakati huo, mbinu za kitaqiyya (kuficha imani kwa sababu za kiusalama), kulea wafuasi maalum, na juhudi za Imam katika kuimarisha misingi ya aqida ya Kishia.

Pia alisisitiza umuhimu wa kufahamu mwenendo wa Ahlul-Bayt (a.s) katika maisha ya leo.

Jamiat Al-Mustafa(s) - Dar-es-Salam | Kikao cha Kielimu: Nafasi ya Imam Hassan Askari(as) katika Kuhifadhi Madhehebu ya Shia Kuendeleza Njia ya Uimamu

Mwisho wa kikao, washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kushiriki mjadala wa kielimu, ambapo walieleza kufurahishwa kwao na manufaa ya kikao hicho, na wakapendekeza kuendelezwa kwa vikao kama hivi ili kuongeza maarifa ya kidini miongoni mwa vijana.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha