Mojawapo ya malengo ya Mitume na Maimam (amani iwe juu yao), ni kusimamisha uadilifu na usawa katika jamii. Kwa mujibu wa Qur'an na hadithi za Maimamu, jamii haiwezi kusimama bila ya uongozi wa Imam Mwadilifu atakayeongoza masuala ya kidini na kijamii. Imam ni mlinzi wa sheria na mwongoza watu kuelekea haki na mafanikio.
Katika hotuba yake, aligusia mazingira ya kisiasa ya wakati huo, mbinu za kitaqiyya (kuficha imani kwa sababu za kiusalama), kulea wafuasi maalum, na juhudi za Imam katika kuimarisha misingi ya aqida ya Kishia.