Waziri wa Elimu ya Juu wa Jimbo la Karnataka, Basavaraj Rayareddy, ameuelezea Uislamu kuwa dini yenye mafundisho yanayosisitiza ubinadamu na kusema kuwa Qur’ani si kwa Waislamu pekee, bali kila mtu anaweza kuisoma. Pia ameeleza nia yake ya kutembelea Makka na kufanya ibada ya Hija.
Wanafunzi wa Chuo cha Kidini cha Khatam al-Nabiyyin (s) mjini Kabul, wakipinga kuendelea kufungwa kwa sehemu kuu za kituo hiki, wamemwambia mwakilishi wa Wizara ya Sheria ya Taliban kwamba kwa karibu miezi miwili sasa wamelazimika kusoma katika maeneo ya wazi, na wameuliza: “Dhambi yetu ni ipi? Je, Mashia hawana haki ya kuwa na Msikiti na shule?”
Kwa kusoma Ziyarat ya Arubaini na kuomboleza kwa ajili ya Imam Hussein (as), Mashia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) mjini Seoul wamehuisha kumbukumbu ya Karbala na kusisitiza kaulimbiu: “Mapenzi ya Hussein yanatuunganisha.”