Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Kipindi muhimu cha DS Podcast kimekaa na Sheikh Yassir Rajabali ili kuchunguza maisha ya Hawza yalivyo kiuhalisia wake. Ni kipindi maalum kilicholinganisha kati ya maisha ya Vyuo Vikuu vya Kisekula (Secular Universities) na Seminari / Hawza za Kiislamu (Islamic Universities or Islamic Seminaries).
Pia yamejadiliwa masuala ya:
Fedha na ndoa, kwa kulinganisha baina ya Vyuo vya Kisekula na Vyuo vya Kiseminari (Hawza), na kuona kama njia hii ya Seminari / Hawza za Kiislamu ni chaguo linalofaa kwa wale wanaotafuta elimu ya kina ya Kiislamu au la.
Sheikh Yassir Rajabali, amesoma Vyuo vyote vya aina mbili. Kwanza amesoma Vyuo vya Kisekula, kisha anasema Nafsi yangu ilivutiwa mno kusoma Vyuo vya Seminari / Hawza za Kidini. Anasema niliamua kujiunga moja kwa moja na Hawzat ili kupata knowledge/ maarifa ya Hawza yenye uwezo wa kunuongoza katika Maisha ya Duniani na hata Maisha ya Akhera.
Akilinganisha Maisha kati ya Maisha ya Hawza na Maisha ya University ya Kisekula amesema:
Watu wengi wanatamani Maisha ya Hawza na wanachukua uamuzi wa kujiunga katika Seminari/ Hawza ili kupata Elimu na Maarifa yenye uwezo mkubwa wa kumuongoza Mwanadamu na hatimaye kuchukua kikamilifu mtindo wa Maisha ya Hawza.
Amesema: Kitu muhimu ambacho mtu anapaswa kukifahamu ni hiki kuwa:
University ya Kisekula haimpi mtu kazi, bali inakupa Elimu basi. Kupitia Elimu kazi utaitafuta mwenyewe kwa Njia yoyote ile itakayowezekana. Hivyo, Mtu hawezi kusema sitaingia katika University / Seminary (Hawza) ya Kiislamu kwa sababu nitapata Elimu tu, huyo atakuwa amekosea kwa sababu Elimu na Maarifa yanayopatikana katika Seminari (Hawza) za Kiislamu zinamuongoza mtu kujipatia kipati halali kwa Njia za halali.
Aidha amesema: Hawza (Seminari ya Kiislamu) pia ni University nyingine, ispokuwa University ya Hawza ni University inayokupa Knowledge/ Maarifa na kuijua Dini yako na Uislamu wako.
Hivyo, Elimu hii ya Hawza inakusaidia mno kuujua Uislamu wako, jambo ambalo huwezi kamwe kulipata katika Elimu zinazotolewa katika Universities / au Vyuo Vikuu vya Kisekula ambavyo havina Elimu za Maarifa ya kukufanya uijue Dini yako na Uislamu wako na uishi maisha mazuri yaliyo katika mtiririko sahihi anaouridhia Mwenyezi Mungu.
Elimu ya Hawza itakupatia Maarifa sahihi yatakayokuongoza kwa Maisha ya hapa Duniani na pia kuelekea Akhera.
Pia, Hawza itakufundisha vizuri thamani ya muda na matumizi mazuri na sahihi ya muda, na namna ya kufaidika na muda ipasavyo.
Hivi sasa, Sheikh Yassir Rajabali ni muhadhiri mashuhuri katika Mimbari za Kiislamu aliyetokea katika University ya Kisekula na kujikuta anachagua na kufadhilisha zaidi Maisha ya Seminari za Kiislamu (kwa maana: Maisha ya Vyuo vya Kihawza).
Your Comment