Kiislamu
-
Sharīatmadār katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili”:
Sayyid Isa Tabatabaei alipuliza roho ya mapambano ndani ya mwili wa jamii ya Kishia / Maadamu kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuwa hai
Balozi wa zamani wa kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: “Ikiwa Imam Musa Sadr alikuwa mwanzilishi wa taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepuliza roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia na kuifanya roho hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wao. Kutokana na jitihada zake, ndipo mapambano ya kisasa ya Lebanon yalipozaliwa - mapambano ambayo baadaye yalifikia kilele chake katika kuunga mkono dhana na malengo ya Palestina.”
-
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Qum atoa wito wa umoja wa wanazuoni na wasomi kwa ajili ya kufanikisha ustaarabu mpya wa Kiislamu
Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Saeed Waezi amesema kuwa kuimarisha umoja na mashauriano kati ya wanazuoni na wasomi wa Kiislamu ni jambo muhimu katika kukabiliana na changamoto za sasa na kufikia malengo makubwa ya ustaarabu mpya wa Kiislamu.
-
Ulinganisho kati ya Maisha ya Seminari (Hawza) za Kiislamu na Maisha ya Vyuo Vikuu vya Kisekula (Kidunia).
Watu wengi wanatamani Maisha ya Hawza na wanachukua uamuzi wa kujiunga katika Seminari/ Hawza ili kupata Elimu na Maarifa yenye uwezo mkubwa wa kumuongoza Mwanadamu na hatimaye kuchukua kikamilifu mtindo wa Maisha ya Hawza.