9 Desemba 2025 - 13:23
Florida Yatangaza “Ikhwan al-Muslimin” na “Baraza la Mahusiano ya Kiislamu-Kimarekani (CAIR)” kuwa Mashirika ya Kigaidi

Jimbo la Florida nchini Marekani limetangaza rasmi kwamba kundi la Ikhwan al-Muslimin na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu–Kimarekani (CAIR) ni mashirika ya kigaidi ya kigeni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Gavana wa Florida ametangaza kuwa makundi haya mawili yameingizwa katika orodha ya mashirika ya kigaidi ndani ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa uamuzi huu, taasisi zote za serikali ya jimbo la Florida zinatakiwa kuchukua hatua za kisheria ili kuzuia aina yoyote ya shughuli zisizo halali za makundi haya; ikiwemo kuzuia mtu au taasisi yoyote inayoyasaidia kifedha. Hatua hii inatajwa kuwa ni ya pili kufanywa na jimbo la Marekani baada ya Texas.

Amri ya Rais Trump

Mwezi Aban 1404, Rais wa Marekani Donald Trump alitoa amri ya kiutendaji (executive order) ambayo ilitoa msingi wa kisheria kwa ajili ya kuziorodhesha baadhi ya matawi ya Ikhwan al-Muslimin kama mashirika ya kigaidi ya kigeni — uamuzi ambao una athari za kisiasa na kiusalama kuanzia Mashariki ya Kati hadi mataifa mengine yenye matawi ya kundi hilo.

Katika taarifa iliyochapishwa na Ikulu ya White House kupitia mtandao wa kijamii “X”, ilielezwa: “Rais Trump amesaini amri ya kiutendaji inayowalazimisha Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Hazina kufanya uchunguzi kuhusu kama baadhi ya matawi ya Ikhwan al-Muslimin yanapaswa kutangazwa kuwa mashirika ya kigaidi ya kigeni na magaidi wa kimataifa maalumu.”

Kwa mujibu wa amri hiyo, Marekani inatumia mamlaka ya sheria za Uhamiaji na Uraia pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Dharura ya Kiuchumi ya Kimataifa ili kuanzisha mchakato wa kuziorodhesha tawi za Ikhwan zilizopo Lebanon, Jordan na Misri.

Madai ya Serikali ya Marekani

Serikali ya Marekani inadai kuwa matawi haya yamehusika katika vitendo vya vurugu, yamechangia hali ya kutokuwa na utulivu, na yanatishia moja kwa moja maslahi ya Washington na washirika wake. Aidha, imeelezwa kuwa baadhi ya matawi ya Ikhwan yalishiriki au kusaidia mashambulizi baada ya tarehe 7 Oktoba 2023 (15 Mehr 1402), na baadhi ya viongozi wao wametuhumiwa kuchochea mashambulizi dhidi ya washirika wa Marekani.

Hatua Zinazofuata

Kwa mujibu wa amri hiyo, Mawaziri wa Mambo ya Nje na Hazina watalazimika kuwasilisha ripoti ya kina ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa amri hiyo. Baada ya hapo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa, zikiwemo:

  • 1_Kufunga au kuzuiwa kwa mali na rasilimali za matawi yanayolengwa
  • 2_Kuzuia miamala au ushirikiano wa kifedha na mashirika hayo
  • 3_Kuchunguza mitandao ya kimataifa ya ufadhili wa makundi hayo
  • 4_Kuweka vikwazo vikubwa vya usafiri na utoaji wa visa kwa viongozi wa makundi hayo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha