Mawasiliano
-
Hafla ya Uzinduzi wa "Mausu‘ah ya Maarifa ya Kishia" Yafanyika / Mfumo wa Kimaarifa wa Kuutambulisha Ushia kwa Msingi wa Akili na Uelewa wa Pamoja
Hafla ya Uzinduzi wa “Mausu‘ah ya Maarifa ya Kishia” Yafanyika / Mfumo wa Kimaarifa wa Kuutambulisha Ushia kwa Msingi wa Akili na Uelewa wa Pamoja wa Kibinadamu
-
Florida Yatangaza “Ikhwan al-Muslimin” na “Baraza la Mahusiano ya Kiislamu-Kimarekani (CAIR)” kuwa Mashirika ya Kigaidi
Jimbo la Florida nchini Marekani limetangaza rasmi kwamba kundi la Ikhwan al-Muslimin na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu–Kimarekani (CAIR) ni mashirika ya kigaidi ya kigeni.
-
Mazungumzo ya Simu kati ya Trump na Maduro Katikati ya Vitisho vya Kijeshi vya Marekani Dhidi ya Venezuela
Rais wa Marekani, Donald Trump, alifanya mawasiliano ya simu na mwenzake wa Venezuela, Nicolás Maduro, na wakajadili uwezekano wa kufanyika kwa mkutano wa ana kwa ana huko Washington, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na New York Times. Mawasiliano haya yalifanyika wakati mvutano ukiwa umeongezeka kufuatia hatua ya Marekani kupeleka majeshi yake katika eneo la Karibi na tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya dhidi ya Maduro-tuhuma ambazo Venezuela huziona kama kisingizio cha kuandaa mabadiliko ya serikali.
-
Athari ya Mawasiliano Bora ya Wazazi kwa Akili ya Kijamii ya Watoto
Mawasiliano bora kati ya wazazi na watoto yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa mtoto. Mtoto anayekulia katika mazingira ambapo mazungumzo yenye kujenga na usikivu makini ni kawaida, baadaye atakuwa na uwezo wa kujenga uhusiano wa afya na thabiti, kufanikisha mafanikio katika mazingira ya kazi na kijamii, na kuishi kama mtu mkarimu na mwenye uelewa wa wengine.
-
Mikakati ya Imam Hadi (a.s) katika Kueneza Mtandao wa Shi'a na Kuimarisha Harakati za Kijamii
Shughuli za Imam Hadi (a.s) zilikuwa na nafasi muhimu katika kuhifadhi utambulisho wa kiakili na imani wa Waislamu wafuasi wa Madhehebu ya Shi'a Ithna Ashari. Uongozi wake wa kiroho na wa fikra kwa Shi'a waliokuwa Samarra, kuimarisha mtandao wa mawasiliano kati ya wafuasi wa Ahlul Bayt(as), na kusimama imara dhidi ya shinikizo la wa Abbasi, ni miongoni mwa huduma muhimu za Imamu Hadi katika maandalizi ya Shi'a kwa zama za Ghaibat Kubwa (Kutoonekana kwa Muda Mrefu).
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s):
Mapinduzi ya Kiislamu ni miale ya fikra ya Ahlul-Bayt (a.s) / Magharibi wanapotosha Uislamu, sisi tunapaswa kusimulia ukweli halisi ulivyo
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mwangaza unaotokana na fikra na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), na kuongeza kuwa: Magharibi wanajitahidi kupotosha taswira ya Uislamu mbele ya dunia, hivyo ni jukumu letu kusimulia ukweli halisi wa Uislamu Sahihi na wa Haki kwa kutumia njia za kisasa za Mawasiliano na Vyombo vya Habari.