Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - "Leo, tarehe 15 April, 2025 limefanyika tukio muhimu na la heshima kupitia Al-Itrah Foundation, Dar -es-Salaam, ikiwakilishwa na Bw. Khomeini Ruhullah, ambapo ilimkabidhi Sheikh Mussa Kundecha, Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zawadi ya Qur'an Tukufu iliyotarjumiwa kwa Tarjama kwa Kalamu ya Marhumu Sheikh Hassan Ally Mwalupa.
Zawadi hii ya Kiroho ni muhimu na ni katika fremu ya kutambua thamani na uzito wa Elimu na Maarifa ya Qur'an Tukufu, na umuhimu wa kuendeleza Umoja na Mshikamano wa Kiislamu baina ya Waislamu.
Your Comment