zawadi
-
Jitahidi; Lakini Usiwe na Pupa Juu ya Riziki
“Jua kwamba riziki iko katika aina mbili: Aina ya kwanza ni riziki ambayo unatakiwa kuitafuta na kuifuata [na ni lazima uitafute]; na aina ya pili ni ile riziki ambayo itakujia yenyewe. Hata kama hutaifuata, yenyewe itakufuata.” Inapaswa kufahamika kwamba katika kutafuta riziki, mwanadamu hapaswi kuwa na pupa, wala kuwa mzembe na mvivu. Kwa hiyo, anapaswa kujituma katika kazi na shughuli zake za kila siku. Hata hivyo, kuna aina ya riziki kama vile urithi, ambayo humfikia mwanadamu bila yeye kufanya juhudi yoyote ya kuipata. Kwa hivyo, mwanadamu hapaswi kukata tamaa anapopungukiwa na riziki ya aina ya kwanza, bali anapaswa kuendelea kujitahidi na kufanya kazi, huku akitarajia pia riziki ambazo humjia bila yeye kuzitafuta au kuzipangia.
-
Wasanii 168 Kushiriki Siku za Utamaduni wa Iran Nchini Urusi
Balozi wa Iran mjini Moscow, Kazem Jalali, ametangaza kuwa wasanii na wanaharakati 168 wa masuala ya utamaduni kutoka Iran watashiriki katika Siku za Utamaduni wa Iran zitakazofanyika katika miji minne ya Urusi mwezi Oktoba.
-
Kitabu cha “Hakimu wa Umma” chazinduliwa Kargil, India
Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Baqir al-Ulum (as) ya Kargil, India, imeandaa mkutano wa kielimu na kifasihi wenye kaulimbiu “Sauti ya Zainab (sa)”, uliowakutanisha wanazuoni, wasomi, washairi, wanafunzi wa vyuo vya dini na vyuo vikuu. Katika hafla hiyo, kitabu “Hakimu wa Umma” kimezinduliwa, huku washindi wa mashindano ya usomaji wa vitabu kwa vijana wakitunukiwa.