3 Juni 2025 - 17:26
UNICEF: Takriban watoto milioni 4 wa Afghanistan hawana fursa ya kupata elimu

UNICEF imetangaza hivi karibuni kuwa takriban watoto milioni 4 nchini Afghanistan hawapati elimu kutokana na uhaba wa shule, huduma za afya, na walimu wenye sifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-  UNICEF imesema hivi karibuni kuwa, kulingana na ripoti ilivyo, takriban watoto milioni 4 nchini Afghanistan hawana fursa ya kupata elimu.

Sababu kuu ya hili ni ukosefu wa miundombinu bora ya shule, maji safi ya kunywa, huduma za afya, pamoja na uhaba wa walimu wenye sifa, hasa walimu wa kike.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limebainisha pia kuwa sababu nyingine ya watoto wengi kuacha shule ni hali ngumu za kiuchumi, ambapo watoto wanapigwa shinikizo la kufanya kazi kwa nguvu kusaidia familia zao.

Zaidi ya hayo, kizuizi kikubwa kwa wasichana kuendelea na masomo yao baada ya darasa la sita ni marufuku iliyowekwa na serikali ya Taliban ya wasichana kusoma.

UNICEF pia iliongeza kuwa, tangu mwanzo wa mwaka wa masomo mpya nchini Afghanistan, ambao huanza mwanzoni mwa mwaka wa kalenda, wasichana wengine 400,000 walipata marufuku ya kwenda shule, na hivyo kwa muda wa miaka mitatu na miezi tisa ya utawala wa Taliban, wasichana milioni 2.2 wamepoteza fursa ya elimu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha