Taliban
-
Mkutano wa wapinzani wa kisiasa wa Taliban nchini Pakistan: Kuunda serikali ya pamoja kutasaidia amani na utulivu wa Afghanistan
Mkutano wa baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Taliban ukiwa na kaulimbiu ya “Kuelekea Umoja na Uaminifu” umefanyika kwa siku mbili mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan. Katika mkutano huu, baadhi ya wasichana wa Shia, wakiwemo Zahra Joyaa, mwanahabari maarufu kutoka Afghanistan, pia walihudhuria.
-
Kiongozi wa kidini wa Waislamu wa Sunni nchini Afghanistan;
Amekosoa sera za Taliban dhidi ya wanawake, akisema: «Mwanamke ni shujaa na ndiye anayezalisha mashujaa wengine»
Hali ilivyo sasa ambapo Taliban nchini Afghanistan wamepunguza haki za wanawake na wasichana kuhusiana na elimu, kazi, na ushiriki katika jamii, kiongozi mmoja wa dini wa Sunni amekosoa waziwazi sera za kutozingatia wanawake za Taliban katika hotuba yake ya umma.
-
Ushinikizi wa Taliban kubadilisha Shule za Kidini kuwa njia pekee ya Elimu kwa Wasichana
Mama mmoja mkoani Nimruz alisema baada ya Mullah kumtaka, alilazimika kuwatoa mabinti zake shuleni na kuwapanga kwenye madarasa ya dini, lakini msaada alioahidiwa haukuwahi kufika. Mama mwingine alisema alipewa masharti: “Ama upeleke binti zako kwenye madarasa ya dini, au hupati chochote.”
-
Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Asilimia 92 ya Watu wa Afghanistan Wanataka Elimu kwa Wasichana Kuendelezwa
Wakati Serikali ya Taliban inaendeleza sera za kuzuia elimu kwa wasichana, ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha wazi kuwa watu wa Afghanistan – wanawake kwa wanaume, wa mjini kwa vijijini – wanataka mabadiliko. Wanataka elimu kwa wasichana, fursa za kazi kwa wanawake, na mustakabali bora kwa jamii nzima.
-
Masomo kwa Wasichana Hayana Nafasi katika Mkakati wa Miaka 5 wa Taliban
Msemaji wa Taliban, alipoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya elimu na masomo ya wasichana katika mkakati huu wa miaka mitano, alisema kuwa suala hilo ni jambo la “kijuujuu” mbele ya mada kuu ya kikao hicho, na akakataa kulijibu.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Pakistan Wawasili Kabul, Afghanistan
Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipokelewa na Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kaimu ya Afghanistan, na kufanya naye mazungumzo. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alipokelewa na Hanafi Wardak, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Taliban.
-
Ahadi Mpya za Taliban / Ufunguzi wa Shule za Wasichana Wategemea "Kibali cha Kisharia"
Zabihullah Mujahid, msemaji wa serikali ya Taliban, ametangaza kuwa mchakato wa kupata “kibali sahihi cha kisharia” kwa ajili ya kufunguliwa tena shule na vyuo vikuu vya wasichana bado unaendelea. Hii ni baada ya zaidi ya miaka minne ya kunyimwa wanawake na wasichana haki ya msingi ya elimu.
-
Umoja wa Mataifa:Katika kuelekea miaka 4 ya utawala wa Taliban, wanawake wa Afghanistan wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa haki za wanawake Duniani
Kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa, katika kuelekea kumbukumbu ya miaka minne tangu Taliban ichukue madaraka nchini Afghanistan, kimetoa taarifa ikikosoa vikali mwenendo wa kundi hilo kuhusu wanawake wa Afghanistan.
-
Kudhibiti Moto wa Misitu na Kutojali kwa Gavana wa Bamiyan Kuhusu Uhamishaji wa Lazima wa Waislamu wa Kishia nchini Afghanistan
Wakati serikali ya muda ya Taliban imetangaza kuwa Gavana wa Mkoa wa Bamiyan, Mawlawi Abdullah Sarhadi, alifika haraka eneo la tukio na kuongoza operesheni ya kuzima moto wa misitu kama ishara ya kujali mazingira, ripoti nyingine zimeripoti uhamishaji wa lazima wa makumi ya familia za Kishia na jamii ya Wahazara kwa amri ya kiongozi huyo huyo wa Taliban – jambo lililosababisha hasira na taharuki kubwa miongoni mwa wananchi na wanaharakati wa kiraia.
-
Mlipuko Mkubwa Watokea Katika Mji wa Bamiyan, Afghanistan
Taarifa kuhusu majeruhi au vifo: Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu kiwango cha majeruhi au uharibifu wa mali, na mamlaka ya polisi ya Taliban mjini Bamiyan haijatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na tukio hili.
-
UNICEF: Takriban watoto milioni 4 wa Afghanistan hawana fursa ya kupata elimu
UNICEF imetangaza hivi karibuni kuwa takriban watoto milioni 4 nchini Afghanistan hawapati elimu kutokana na uhaba wa shule, huduma za afya, na walimu wenye sifa.
-
Balozi wa Taliban nchini Qatar: Emirate ya Kiislamu ni ukweli wa Afghanistan / Iran na India hawaiweki Taliban tena chini ya ushawishi wa Pakistan
Suhail Shahin, balozi wa Taliban nchini Qatar, katika mazungumzo na kituo cha Al Jazeera amesema kwamba Iran na India walidhani Taliban ni tegemezi wa Pakistan, lakini sasa wamegundua kuwa fikra hiyo si ya kweli.
-
Kuendelea kuwepo kwa Marekani nchini Afghanistan kinyume na misimamo rasmi ya pande husika / Ujasusi na vitisho vya Marekani kwa nchi za eneo
Ingawa Marekani kwa dhihiri imeondoa majeshi yake kutoka Afghanistan, ripoti na kauli za Donald Trump zinaonyesha kuwa msingi mmoja wa kimkakati bado uko chini ya udhibiti wa Marekani nchini humo. Washington inatumia kambi hii kufanikisha malengo kama vile ufuatiliaji wa taarifa za kijasusi kuhusu Iran, China na Urusi, pamoja na kuhifadhi ushawishi wake katika Asia ya Kati.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Taliban akiwa Tehran: Haki ya maji ya Iran imekuwa ikitiririka kwa mwezi mmoja sasa
Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Muda ya Afghanistan, amesema saa chache zilizopita katika “Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran” kwamba: “Kwa mwezi mmoja sasa, haki ya maji ya Iran kutoka Afghanistan imekuwa ikielekezwa kuelekea Sistan na Baluchestan.”