Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mujahid alisema kuwa masuala kama vile heshima, hijabu na namna ya kutembea kwa wasichana ni mada kuu zinazojadiliwa na wanazuoni wa kidini, na hadi pale watakaporidhishwa, uamuzi wa mwisho hautachukuliwa.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Mujahid alieleza kuwa kutakuwa na mabadiliko katika muundo wa serikali ya Taliban, ambapo cheo cha “msimamizi (sarparast)” kitaondolewa katika baraza la mawaziri. Alidai kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi na kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi, na kuanzia sasa Taliban watakuwa “na wajibu kamili” kwa wananchi wa Afghanistan.
Kuhusu suala la kutambuliwa kimataifa, Mujahid alisema kuwa tatizo lililopo linatokana na sera za kivita za mataifa ya kigeni dhidi ya Afghanistan, na akasisitiza kuwa milango ya serikali ya Taliban ipo wazi kwa watu wenye uadilifu na sifa, hata wale ambao hawajawahi kuwa wanachama wa kundi hilo.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuwa ahadi za mara kwa mara za Taliban kuhusu kufunguliwa kwa shule za wasichana hazijawahi kutekelezwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Mamilioni ya wasichana wa Afghanistan bado wananyimwa haki ya elimu, na kile kinachoitwa “kibali cha kisharia” kinaonekana zaidi kama kisingizio kipya cha kuchelewesha na kuendeleza kunyimwa kwa wanawake fursa ya masomo.
Your Comment