26 Agosti 2025 - 17:13
Masomo kwa Wasichana Hayana Nafasi katika Mkakati wa Miaka 5 wa Taliban

Msemaji wa Taliban, alipoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya elimu na masomo ya wasichana katika mkakati huu wa miaka mitano, alisema kuwa suala hilo ni jambo la “kijuujuu” mbele ya mada kuu ya kikao hicho, na akakataa kulijibu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Zabihullah Mujahid, msemaji wa Serikali ya Taliban, katika mkutano wa moja kwa moja na waandishi wa habari leo (Jumanne: 26-08-2025), alieleza kuhusu mkakati wa miaka mitano wa Serikali ya mpito kwa ajili ya maendeleo ya Afghanistan.

Mujahid alibainisha kuwa kuandaliwa kwa mkakati huu kumetokana na agizo la kiongozi wa Taliban, na umelenga katika kutumia uwezo na rasilimali za ndani ili kufikia malengo makuu ya kitaifa ya Afghanistan.

Msemaji huyo wa Taliban alisema kuwa hati hii ina nguzo kuu tatu: utawala bora na uhusiano wa kimataifa, usalama na nidhamu ya kijamii, pamoja na uchumi na maendeleo ya kijamii. Aidha, inajumuisha maeneo kumi muhimu na programu kumi na tano za kipaumbele.

Baada ya kuwasilisha mkakati huu wa miaka mitano, Mujahid alijibu maswali ya waandishi wa habari.

Hata hivyo, alipoulizwa tena kuhusu nafasi ya elimu ya wasichana ndani ya mkakati huu, alisema kuwa ni jambo la kijuujuu na hakutoa jibu lolote. Badala yake, alitoa kauli ya jumla akisema kuwa elimu, afya na sekta nyingine zimo ndani ya mkakati huo.

Mwisho wa kikao hicho cha habari, Mujahid kwa mara nyingine aliepuka kujibu swali la waandishi kuhusu elimu na masomo ya wasichana nchini Afghanistan.

Ni vyema kukumbuka kuwa, tangu Taliban walipochukua madaraka Afghanistan katika kiangazi cha mwaka 1400 Hijria Shamsi (Agosti 2021), wamesitisha masomo ya wasichana na wanawake kuanzia kidato cha sita na kuendelea, na pia wamewazuia kujiunga na vyuo vikuu hata katika fani zilizotengwa mahsusi kwa wanawake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha