Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulimalizika kwa sare ya bao 1–1, lakini katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwa hamasa na nidhamu ya hali ya juu, timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Nyabuningi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya timu ya Shule ya Imam Zaynul Aabidin (a.s).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Katika mfululizo wa michezo ya kirafiki, mchezo wa marudiano kati ya timu ya Shule ya Imam Zaynul Aabidin (a.s) na timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Nyabuningi umechezwa kwa ushindani mkubwa.
Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulimalizika kwa sare ya bao 1–1, lakini katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwa hamasa na nidhamu ya hali ya juu, timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Nyabuningi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya timu ya Shule ya Imam Zaynul Aabidin (a.s).
Timu zote mbili zilionesha mchezo mzuri wenye nidhamu na ushindani wa kiurafiki, na hivyo kuonyesha mfano wa umoja na maadili bora ya michezo.
Uongozi wa Shule ya Imam Zaynul Aabidin (a.s) umeipongeza timu pinzani kwa ushindi huo, huku ukitoa pongezi na shukrani kwa wachezaji wake kwa kujituma na kuonyesha mchezo wa hali ya juu. Wamesisitiza kuwa lengo kuu la michezo hii ni kujenga ushirikiano, nidhamu, na kukuza vipaji vya michezo miongoni mwa wanafunzi.
Your Comment