Miaka 10
-
Imamu Jamaa wa Zamani wa Masjid al-Haram (Msikiti Mtukufu wa Makkah) Aachiwa Huru Baada ya Miaka 7 Gerezani Saudi Arabia
Sheikh Saleh Al-Talib mnamo mwaka 2018 katika moja ya khutba zake alipinga maonesho ya muziki (konseti) na mikusanyiko ya kijinsia iliyochanganyika, jambo lililosababisha kutoridhishwa na viongozi wa Saudia na pia shinikizo kutoka kwa taasisi za kiserikali zinazohusiana na Mamlaka Kuu ya Burudani ya Saudi Arabia, na hatimaye kusababisha kukamatwa kwake.
-
Meja Jenerali Musawi: Jeshi la Ukombozi litatoa jibu lililo juu ya fikra za waonevu (waovu)
Rais wa Makao Makuu ya Majeshi ya Ulinzi wa Iran amesema: Tunawapa uhakika wananchi wa Iran wenye heshima na ushujaa kuwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutegemea uwezo wao, ubunifu na mshangao wa kimkakati, viko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya madhalimu na waonevu wa dunia kwa majibu ya wakati muafaka, makali, ya kujutia na yaliyo zaidi ya fikra zao.
-
Waislamu wawili kati ya watatu nchini Ufaransa ni waathirika wa ubaguzi wa rangi
Chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa inaongezeka, na asilimia 66 ya Waislamu wa nchi hiyo wamekuwa waathirika wa ubaguzi na chuki za kijinsia na kikabila katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
-
Sehemu ya Kwanza:
Miaka 120 ya Mapambano ya Familia ya Khamenei | Kizazi cha Upinzani na Mapambano | “Ninajivunia Kwamba Huyu Mtu Mashuhuri ni Babu Yangu"
Msimamo wa kupinga dhuluma na mapambano umekuwa miongoni mwa sifa kuu za familia ya Khamenei tangu karne zilizopita hadi sasa. Ingawa hakuna historia iliyoandikwa rasmi kuhusu mapambano ya familia hii, kuna ushahidi wa kihistoria na vielelezo vya wazi vinavyoonyesha kuwepo kwa historia ya miaka 120 ya mapambano yao.
-
Masomo kwa Wasichana Hayana Nafasi katika Mkakati wa Miaka 5 wa Taliban
Msemaji wa Taliban, alipoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya elimu na masomo ya wasichana katika mkakati huu wa miaka mitano, alisema kuwa suala hilo ni jambo la “kijuujuu” mbele ya mada kuu ya kikao hicho, na akakataa kulijibu.
-
Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti wa Tanzania Dr.Abubakar Zubair: Historia ya Mafanikio na Maboresho Makubwa
Miradi mikubwa yenye thamani ya mabilioni imetekelezwa katika mikoa mbalimbali, huku maboresho ya kiutawala na ya kimuundo yakifanikishwa, ikiwemo kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti, JUWAKITA na JUVIKIBA, pamoja na mabadiliko ya Katiba ya BAKWATA ili kuendana na mahitaji ya sasa.