Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Sheikh Saleh Al-Talib, aliyekuwa imamu wa zamani wa Msikiti Mtukufu wa Makkah (Masjid al-Haram), baada ya kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka saba gerezani, hatimaye ameachiwa huru, lakini bado yupo chini ya kifungo cha nyumbani na analazimika kuvaa kifaa cha kielektroniki mguuni.
Sababu ya kukamatwa kwa Saleh Al-Talib inarejea mwaka 2018, ambapo katika moja ya khutba zake alisema kuwa ni jambo la kulaumiwa kidini iwapo wanawake na wanaume watakuwa pamoja katika maonesho ya muziki na mikusanyiko mingine na kufurahia matukio hayo.
Khutba hiyo ya imamu wa zamani wa Masjid al-Haram ilisababisha kutoridhishwa na viongozi wa Saudia pamoja na shinikizo kutoka taasisi za kiserikali zinazohusiana na Mamlaka Kuu ya Burudani ya Saudi Arabia, na hatimaye kusababisha kukamatwa kwake.
Your Comment