Makkah
-
Imamu Jamaa wa Zamani wa Masjid al-Haram (Msikiti Mtukufu wa Makkah) Aachiwa Huru Baada ya Miaka 7 Gerezani Saudi Arabia
Sheikh Saleh Al-Talib mnamo mwaka 2018 katika moja ya khutba zake alipinga maonesho ya muziki (konseti) na mikusanyiko ya kijinsia iliyochanganyika, jambo lililosababisha kutoridhishwa na viongozi wa Saudia na pia shinikizo kutoka kwa taasisi za kiserikali zinazohusiana na Mamlaka Kuu ya Burudani ya Saudi Arabia, na hatimaye kusababisha kukamatwa kwake.
-
Mwenyekiti wa Baraza la Ulamaa wa Pakistan: Mahali pa mwisho pa mradi wa "Israeli Kubwa" ni Makka na Madina
Mkuu wa Baraza la Ulamaa wa Pakistan alionya kwamba mradi wa "Israeli Kubwa" unatafuta udhibiti wa mwisho juu ya Madina na Makka.
-
Je, Makaburi ya Baqii yalizingirwa na kuharibiwa (kubomolewa) na kina nani? | Matukio yalivyotendwa katika uharibifu wa Baqii
Mnamo mwaka wa 1220 A.H., Mawahabi waliutwaa mji huo baada ya kuzingirwa kwa mwaka mmoja na nusu na kwa sababu ya njaa huko Madina. [25] Kulingana na vyanzo vilivyopo, baada ya kujisalimisha kwa Madina, Saud bin Abdul Aziz alitaifisha mali yote iliyokuwa kwenye hazina ya Madhabahu ya Mtume na pia akaamuru kuharibiwa kwa majengo na majumba yote ya Madina, pamoja na makaburi ya Baqi.[26]
-
Imetolewa Katika Mkutano wa Ukosoaji wa Mfululizo wa Muawiyah:
Mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, Ni utekelezaji wa amri za Kiwahabi / Ili kuvutia hadhira badala ya kusimulia Historia halisi!
Katika mkutano wa mapitio ya mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, wataalamu walizingatia lengo kuu la mfululizo huu kuwa ni utakaso wa Bani Umaiyya na Muawiyah, na ni upotoshaji wa Historia kwa kupendelea Uwahabi, na ni katika kukamilisha mradi wa migogoro baina ya Shia-Sunni.