Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Mnamo mwaka wa 1220 A.H., Mawahabi waliutwaa Mji wa Madina baada ya kuuzingirwa kwa mwaka mmoja na nusu na kwa sababu ya kusambaa kwa baa la njaa katika Mji huo wa Madina. [1] Kulingana na vyanzo vilivyopo, baada ya kujisalimisha kwa Madina, Saud bin Abdul Aziz alitaifisha mali yote iliyokuwa kwenye hazina ya Madhabahu ya Mtume na pia akaamuru kuharibiwa kwa majengo na majumba yote ya Madina, pamoja na makaburi ya Baqi.[2]. Kwa kuzingatia tukio hili, Haram (Madhabahu) za Maimamu wanne wa Kishia pamoja na Kuba iliyohusishwa na Fatimah (s.a), ambayo iliitwa Bayt Al-Ahzan, iliharibiwa au kuharibiwa vibaya sana katika shambulio la kwanza la Kiwahabi mwaka 1220 Hijria [3].
Baada ya tukio hili, Serikali ya Ottoman ilituma jeshi kuiteka Madina na kuirudisha kutoka mikononi mwa Mawahabi, na katika Mwezi wa Dhul-Hijjah 1227 Hijria, iliirudisha Madina toka mikononi mwao na kuidhibiti. Kwa hiyo, 1234 AH [4] Mahmud II, Sultani wa 30 wa Ottoman, aliamuru kujengwa upya kwa Madhababu (Haram) zote za Baqii zilizokuwa zimebomolewa na Mawahhabi.
Mawahabi waliishambulia tena Madina katika Mwezi wa Safar 1344 Hijiria [5]. Katika shambulio hilo, uharibifu mkubwa ulisababishwa kwenye Madhabahu (Haram) ya Mtume na sehemu zingine za Kimadhehebu [3]. Miezi saba baadaye, katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ya Mwaka 1344 AH, Sheikh Abdullah bin Bulayhid (1284 - 1359 AH), ambaye alikuwa Hakimu wa Mahakamimu wa Makka kuanzia Mwaka 1343 hadi 1345 AH, [6] aliingia katika Mji wa Madina, na kwa kuegemea katika kura ya maoni (au Fat'wa) kutoka kwa Mamufti wa Madina (wa kiwahhabi), aliamuru (alitoa hukumu ya) uharibifu mkubwa (ufanyike kwenye Makaburi ya Baqii walipozikwa kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w.w) [7].
Mnamo tarehe 8 Shawwal 1344 Hijria, athari zote za Kihistoria za Baqii, yakiwemo Makaburi ya Baqii, yaliharibiwa (na kufyekwa) kupitia Fat'wa ya Sheikh Abdullah Bulayhid, Hakimu wa Mahakimu wa Saudia, akiegemea kwenye Fat'wa ya Mamufti wa kiwahhabi wa Madina [8].
Mamufti 15 wa Madina [9] katika Fat'wa yao (ya kiwahhabi) iliyotajwa hapo juu, kwa kauli moja walitangaza kuharamisha ujenzi wa Makaburi (kwamba ni haram kujengea kaburi na kuwlifanya kaburi liwe ndani ya jengo kama lilivyo kaburi Tukufu la Mtume Muhammad s.a.w.w, hivyo wakaamuru Makaburi yote yaliyo ndani ya majengo (au yaliyojengewa) kuharibiwa na kubomoa majengo hayo mara moja [10].
La ajabu sana ni hili kwamba: Kaburi la Mtume (s.a.w.w) limejengewa na lipo ndani ya Dharihi, Dunia haikuona Mawahhabi wakithubutu kulibomoa Kaburi Tukufu la Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w), hali ya kuwa Madina tayari ilishaangukia mikononi mwao na mpaka leo hii iko chini ya udhibiti wao!. Fat'wa yao ya kiwahhabi ilihusu Makaburi ya Baqii yaliyojengewa kama lilivyo jengewa leo hii Kaburi la Mtume (s.a.w.w) na kuwa ndani ya Msikiti, jambo ambalo kwa akili za kiwahhabi ni haram kaburi kuwa ndani ya jengo, au Msikiti , yote hiyo kwao ni anuani moja ya kujengea kaburi!.Na hilitunamuachia kila mwenye akili timamu kutathmini akili na mienendo za kiwahhabi na itikadi zao zilizotofauti na Uislamu!.Ukitaka kujua itikadi za kiwahhabi ni itikadi za kihayawani, tizama itikadi hii ya kujengea makaburi wanavyoenda nayo kibubusa, kaburi na baba wa itikadi za kufurutu ada za kiwahhabi ambaye Ibn Taimiyya limejengewa!, Mawahhabi wafanya ugaidi kote duniani hatuwaoni wakienda kufanya ugaidi wa kulibomoa kaburi hilo na kulisawazisha chini ya ardhi ili watimize itikadi hiyo ya kiwahhabi ya uharamu wa kujengea kaburi!. Tizama kaburi hilo la Ibn Taymiyya hapo juu na hapa chini:
Kaburi la Ibn Taymiyya ambaye ndiye msingi wa itikadi za kiwahhabi, likiwa limejengewa!
Hawabomi kaburi hili la Ibn Taimiyya wanaliheshimu sana, lakini walienda katika Mji Mtukufu wa Madina kunajisi Makaburi Matukufu ya Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)!. Hii ni sio itikadi, bali ni chuki kubwa dhidi ya kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Bali hata Kaburi Tukufu la Mtume Muhammad (s.a.w.w) limejengewa na liko ndani ya Msikiti, jambo ambalo kwa Mawahhabi ni haram maana huko ni kujengea kaburi na Fatwa zao zinaharamisha, lakini hawaligusi Kaburi Tukufu la Mtume (s.a.w.w) mpaka leo hii maana wanajua utakuwa ndio mwisho wao, hakuna Muislamu duniani atawaridhia kuona Mawahhabi wanalinajisi na kulivunjia heshima Kaburi Tukufu la Mtume wao Muhammad (s.a.w.w) kupitia Fat'wa zao feki na ya kihayawani na kiwahhabi.
Kaburi Tukufu la Mtume Muhammad (s.a.w.w) likiwa limejengewa na likiwa ndani ya - Masjid ya Mtume (s.a.w.w) maarufu kama - Masjid al-Nabawi, Madina
Katika Picha hii, unaweza kuiona Quba ya Kijani (The Green Dome) ya Kaburi la Mtume Muhammad (s.a.w.w). Huu ni Msikiti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ndani yake au chini ya hiyo Quba ya Kijani, ndipo lilipo Kaburi Tukufu la Mtume wa Uislamu na Waislamu Muhammad (s.a.w.w).
Hata hivyo, kinyume na imani ya Mawahabi, kwa mujibu wa imani maarufu ya Sunni na Shia, ujenzi wa Makaburi (au kujengea Makaburi na yakawa ndani ya jengo au ndani ya Msikiti au Misikiti) haupingani na imani ya Kiislamu (na wala sio Haram), na kuzuru Makaburi ya Wakubwa wa Kidini na Makaburi ya Waumini kunapendekezwa katika Uislamu (kwa maana ni Mustahabu) [11].
Mfalme Abdulaziz, Mwanzilishi wa Ufalme wa ukoo wa Al-Saud nchini Saudi Arabia
Kulingana na hati zilizopo (au maandiko yaliyopo), baada ya maangamizi hayo yaliyofanywa na Mawahhabi kwa kuytafyeka makaburi ya Baqii na kuzipoteza athari zote za Baqii na kuyanajisi na kuyavunjia heshima Makaburi ya watukufu wa Ahlubayt (s.a.w.w) katika ardhi ya Baqii, Mfalme Abdulaziz, Mfalme wa Saudi Arabia (na Mwanzilishi wa Ufalme wa Kisaudia), katika barua yake ya tarehe 12 Shawwal 1344 AH ambayo alimuandikia Kadhi wa Makadhi wa Saudia, Sheikh Abdullah bin Bulayhid (1284 - 1359 AH), alisifu sana matendo yake katika suala hili [12].
Rejea:
1-↑ Jabrati, Maajabu ya Mambo ya Kale, Dar Al-Jeel, Juzuu ya 3, uk.91.
2-↑ Ghalib, I Min Akhbar Al-Hijaz wa Al-Najd, 1395 AH, uk. 104. Ma'jara, Al-Baqi Qissat al-Tadmir, 1411 AH, uk. 84. Jabrati, Aja'ibul - A'thar (Maajabu ya Mambo ya Kale), Dar Al Jail, Juzuu. 3, uk. 91. ↑ Jabrati, Maajabu ya Mambo ya Kale, Dar al-Jail, Juzuu ya 3, uk.91.
3-↑ Jabrati, Aja'ibul - A'thar (Maajabu ya Mambo ya Kale), Dar Al Jail, Juzuu. 3, uk. 91.
4-↑ Jafarian, Vitabu hamsini vya safari za Hajj Qajar, 1389, Juzuu ya 3, uk.196.
5-↑ Ma'jara, Al-Baqi Qissat al-Tadmir, 1411 AH, uk. 113-139; Amini, Baqi al-Gharqad, 1386 Shamsia, Ukurasa wa 49.
6-↑ 31-Zarkali, Al- A'lam, 2002, Juzuu ya 4, uk.91.
7-↑ Balaghi, Al-Aradu Ala' al-Wahhabiyyah, 1419 AH, ukurasa wa 41-39; Ma'jara, Al-Baqi Qissat al-Tadmir, 1411 AH, uk. 113-139; Amini, Baqi al-Gharqad, 1386 Shamsia, Ukurasa wa 49.
8-↑ Ma'jara, Al-Baqi Qissat al-Tadmir, 1411 AH, uk. 113-139; Amini, Baqi al-Gharqad, 2006, p. 49; Najmi, Historia ya Madhabahu ya Maimamu,1386 Shamsia, ukurasa wa 51.
9-↑ Balaghi, Al-Aradu Ala' al-Wahhabiyyah, 1419 AH, Ukurasa wa 45.
10-↑ Balaghi, Al-Aradu Ala' al-Wahhabiyyah, 1419 AH, pUkurasa wa 40.
11-↑ Madani, Al-Tarikh Al-Amin, 1418 AH, ukurasa wa 431-450; Amini, Baqi al-Gharqad, 1386 Shamsia, Ukurasa wa 12.
12-↑ Al-Assaf, "Abdullah bin Suleiman al-Bulayhid... Al-Qadi wal-Mustasharu fi zaman al-taasis (Hakimu - Kadhi - na Mshauri katika zama za kuasisiwa kwa ufalme wa saudia)".
Your Comment