Mnamo mwaka wa 1220 A.H., Mawahabi waliutwaa mji huo baada ya kuzingirwa kwa mwaka mmoja na nusu na kwa sababu ya njaa huko Madina. [25] Kulingana na vyanzo vilivyopo, baada ya kujisalimisha kwa Madina, Saud bin Abdul Aziz alitaifisha mali yote iliyokuwa kwenye hazina ya Madhabahu ya Mtume na pia akaamuru kuharibiwa kwa majengo na majumba yote ya Madina, pamoja na makaburi ya Baqi.[26]
Historia inaonyesha kuwa, katika tukio hilo la kusikitisha, lililotokea tarehe 8 Mfunguo Mosi Shawwal 1345 Hijria (1925 Miladia) Mawahabi wa Saudi Arabia walibomoa makaburi ya Ahlul-Bayt -a.s- wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambayo yanapatikana katika ardhi ya Baqi’i, katika Mji Mtakatifu wa Madina.