14 Oktoba 2025 - 20:43
Uharibifu wa Makaburi ya Jannat al-Baqi‘ - Historia na Umuhimu Wake

Uharibifu wa Jannat al-Baqii umeacha doa lisilofutika katika historia ya Uislamu. Makaburi haya hayakuwa tu sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria, bali pia yalikuwa alama ya mapenzi na heshima kwa watu waliotumikia Uislamu kwa ikhlasi na kujitolea. Leo hii, Waislamu kote duniani wanaendelea kuomba urejesheaji Heshima na Staha inayostahili kwa Makaburi haya matukufu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Makaburi ya Jannat al-Baqi‘ yaliyoko katika mji mtakatifu wa Madina al-Munawwara yalinajisiwa, kuvunjiwa jeshima,, na kubomolewa na majeshi ya Mawahhabi wa Saudi tarehe 8 Shawwal, mwaka 1344 Hijria, ambayo inasadifiana na Aprili 21, 1926 (na baadhi ya vyanzo vinasema ilikuwa Aprili 22). Tukio hili linaendelea kukumbukwa hadi leo kama moja ya matukio yenye kuleta majonzi makubwa katika historia ya Uislamu. Ukisoma Historia ya Uislamu ilivyo, utaona ni jinsi gani hawa Mawahhabi walivyokuwa na Chuki dhidi ya Ahlul-Bayt wa Mtume (saww) kiasi kwamba Chuki ya kiupofu na waliyoirithi toka kwa Bani Umaiyyah ilipowafikisha mpaka kuvunja vunja makaburi Matukufu ya watu Watukufu wa Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Mtukufu Muhammad (saww), huku wakisingizia ATI huo ndio Uislamu na ndio itikadi ya Kiislamu ilivyo! Ajabu wakati huo Kaburi Tukufu la Mtume Muhammad (saww) limejengewa lakini hakuna Muwahhabi aliyethubutu kulibomoa, na tangu Zama hizo Mamlaka ya eneo Kaburi lilipo iko mikononi mwao!. Eneo la Baqii wakadai wanatekeleza itikadi yao ya kiupofu na Ukosefu wa Maarifa, lakini eneo lilipo Kaburi Tukufu la Mtume (saww) kwa maana hapo itikadi yao haina Mahusiano napo! Ala kuli Hali, Allah atawaonyesha Madhalimu wakati wao ukifika ni mgeuko upi wanaogeuka.

Historia Fupi ya Jannat al-Baqii

Jannat al-Baqi‘ ni mojawapo ya makaburi matakatifu zaidi katika Uislamu, likiwa ni sehemu ya mapumziko ya amani kwa watu mashuhuri wa familia ya Mtume (s.a.w.) na Masahaba wake wema.
Miongoni mwa waliolazwa hapa ni:

1_Imam Hasan ibn Ali (a.s.)

2_Imam Zaynul Aabidin (a.s.)

3_Imam Muhammad al-Baqir (a.s.)

4_Imam Ja‘far al-Sadiq (a.s.)

5_Wanafamilia wengine na Masahaba wakubwa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Matukio Muhimu ya Kihistoria

1. Uharibifu wa Kwanza (1806 / 1221 A.H)

Uharibifu wa kwanza ulifanywa na utawala wa kwanza wa Saudi-Wahhabi baada ya kuuteka Mji wa Madina.

Katika kipindi hiki, Kuba na majengo yaliyokuwa yamejengwa juu ya makaburi ya watu watakatifu yalivunjwa kwa madai ya kupinga "Ushirikina!".

2. Ujenzi Upya na Enzi za Waothmani

Baada ya Dola ya Ottoman kurejesha udhibiti wa Madina, makaburi hayo yalijengwa upya kwa heshima kubwa.
Majengo mapya yalikuwa na usanifu wa kipekee, yakionyesha utukufu wa Ahlul Bayt (a.s.) na historia ya Kiislamu.

3. Uharibifu wa Pili (1925–1926 / 1344 A.H.)

Baada ya Mfalme Abdulaziz ibn Saud kuchukua udhibiti wa Madina, utawala mpya wa Saudi-Wahhabi uliamuru kubomolewa tena kwa makaburi na kuba zote zilizokuwapo ndani ya Jannat al-Baqi‘.
Tukio hili lilifanyika tarehe 8 Shawwal, na linakumbukwa kila mwaka na Waislamu wengi - hasa Wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s.) -kama “Youm al-Gham” yaani “Siku ya Huzuni”.

Uharibifu wa Makaburi ya Jannat al-Baqi‘ - Historia na Umuhimu Wake

Mpangilio wa Makaburi Matukufu ndani ya Baqi‘

Ndani ya eneo la Jannat al-Baqi‘, Makaburi ya Maimamu na watu mashuhuri wa familia ya Mtume (s.a.w.w) yamepangwa kwa mpangilio maalum kama ifuatavyo:

1_Kaburi lililopo peke yake (katika Picha hiyo) ni la Bibi Fatima bint Asad (r.a.), Mama yake Imam Ali ibn Abi Talib (a.s).

  • 2_Makaburi manne yaliyosalia, yanayoonekana kuwa karibu karibu, ni ya:
    1. Imam Hasan al-Mujtaba (a.s.) - Upande wa kushoto,
    2. Imam Zaynul Aabidin (a.s),
    3. Imam Muhammad al-Baqir (a.s.),
    4. Imam Ja‘far al-Sadiq (a.s.) - Upande wa kulia.

Mpangilio huu ulihifadhiwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (amani iwe juu yao) na unaendelea hadi Leo hii kuhifadhiwa kwa heshima kubwa, na unaendelea kuwa sehemu muhimu ya urithi wa Kiislamu kabla ya kubomolewa makaburi ya Baqii na hata baada ya kubomolewa.

Mwisho kabisa:

Uharibifu wa Jannat al-Baqii umeacha doa lisilofutika katika historia ya Uislamu. Makaburi haya hayakuwa tu sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria, bali pia yalikuwa alama ya mapenzi na heshima kwa watu waliotumikia Uislamu kwa ikhlasi na kujitolea.
Leo hii, Waislamu kote duniani wanaendelea kuomba urejesheaji Heshima na Staha inayostahili kwa Makaburi haya matukufu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha