Bani Umaiyyah
-
Uharibifu wa Makaburi ya Jannat al-Baqi‘ - Historia na Umuhimu Wake
Uharibifu wa Jannat al-Baqii umeacha doa lisilofutika katika historia ya Uislamu. Makaburi haya hayakuwa tu sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria, bali pia yalikuwa alama ya mapenzi na heshima kwa watu waliotumikia Uislamu kwa ikhlasi na kujitolea. Leo hii, Waislamu kote duniani wanaendelea kuomba urejesheaji Heshima na Staha inayostahili kwa Makaburi haya matukufu.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt(AS):
Ghadir inachukuliwa kuwa ni harakati ya kuunganisha Uislamu | Kama Kusingekuwa na Ghadir, Uislamu Halisi ungeamizwa na Bani Umaiyya na Bani Abbas
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS): Kabla ya Mapinduzi, walikisema haiwezekani kuwepo kwa Mapinduzi ya Kiislamu, na wanachuoni hawakufikiri kwamba mabadiliko makubwa yangetokea nchini Iran, bali Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwepo na yalishinda, na hayo yalikuwa ni Mapinduzi yaliyoongozwa na Kiongozi Muadhamu, na kila kitu kuhusu Mapinduzi hayo kilikuwa ni ufunuo kwa dini, kwamba hayo si chochote ila ni muujiza na kazi ya Mwenyezi Mungu.
-
Imetolewa Katika Mkutano wa Ukosoaji wa Mfululizo wa Muawiyah:
Mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, Ni utekelezaji wa amri za Kiwahabi / Ili kuvutia hadhira badala ya kusimulia Historia halisi!
Katika mkutano wa mapitio ya mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, wataalamu walizingatia lengo kuu la mfululizo huu kuwa ni utakaso wa Bani Umaiyya na Muawiyah, na ni upotoshaji wa Historia kwa kupendelea Uwahabi, na ni katika kukamilisha mradi wa migogoro baina ya Shia-Sunni.