17 Juni 2025 - 17:21
Ghadir inachukuliwa kuwa ni harakati ya kuunganisha Uislamu | Kama Kusingekuwa na Ghadir, Uislamu Halisi ungeamizwa na Bani Umaiyya na Bani Abbas

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS): Kabla ya Mapinduzi, walikisema haiwezekani kuwepo kwa Mapinduzi ya Kiislamu, na wanachuoni hawakufikiri kwamba mabadiliko makubwa yangetokea nchini Iran, bali Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwepo na yalishinda, na hayo yalikuwa ni Mapinduzi yaliyoongozwa na Kiongozi Muadhamu, na kila kitu kuhusu Mapinduzi hayo kilikuwa ni ufunuo kwa dini, kwamba hayo si chochote ila ni muujiza na kazi ya Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Ayatollah Reza Ramezani alihutubia wafanyakazi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (as) asubuhi ya leo, akizungumzia nafasi ya Mtume (s.a.w.w) mbele ya Mwenyezi Mungu, na akasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) heshima maalum miongoni mwa Mitume wote (a.s) wa Mwenyezi Mungu.

Ghadir inachukuliwa kuwa ni harakati ya kuunganisha Uislamu | Kama Kusingekuwa na Ghadir, Uislamu Halisi ungeamizwa na Bani Umaiyya na Bani Abbas

Licha ya utukufu ambao Mwenyezi Mungu anampa Mtume (s.a.w.w) ndani ya Quran, Mtukufu Mtume (saww) anatishiwa katika sehemu tatu ndani ya Quran. Moja ya vitisho hivyo ni kuhusiana na wajibu wa Mtume (saww) wa kufikisha ujumbe wa Tauhidi kama ilivyoelezwa katika Aya ya 65 ya Sura Az-Zumar:

«وَلَقَدْ أُوحِیَ إِلَیْکَ وَإِلَی الَّذِینَ مِنْ قَبْلِکَ لَئِنْ أَشْرَکْتَ لَیَحْبَطَنَّ عَمَلُکَ وَلَتَکُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِینَ» 

"Hakika imefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako ya kwamba ukimshirikisha Mwenyezi Mungu amali zako zote zitapotea bure na utakuwa miongoni mwa walio khasirika"

Aliendelea: Tishio la pili kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Mwenyezi Mungu lilikuwa ni kuhusu kutoongeza au kupunguza maneno ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akamwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akisema kwamba huna haki ya kuongeza au kupunguza hata neno moja la maneno yangu. Katika Aya ya 44 ya Sura Al-Haqqa imeelezwa: 

«وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَیْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِیلِ»

"Na lau angeli tuzulia baadhi ya kauli kuwa ni uwongo".

Tishio la tatu lilikuwa kuhusu tangazo la Uimamu na Wilaya. Mwenyezi Mungu alisema katika aya ya 67 ya Surat al-Maidah:

«یَا أَیُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَیْکَ مِنْ رَبِّکَ ۖ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّهُ یَعْصِمُکَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا یَهْدِی الْقَوْمَ الْکَافِرِینَ»

"Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako [kuhusu uimam na uongozi wa Ali ibn Abi Talib, Amirul-Muuminina (amani iwe juu yake)]; na usipoifanya, basi hujafikisha ujumbe wa Mungu. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri".

Ghadir, Mwendelezo wa Risala (Ujumbe); A'shura, Muendelezo wake

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) aliuchukulia Uislamu kuwa unahitaji mwongozo na maelezo yenye kuendelea na akasema: Kazi zote za Mtume (saww) isipokuwa kwa "Wahyi" zilihamishiwa kwa Imam Maasum (as) baada yake. Kuwepo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kuhifadhi Quran na mafundisho yake, hivyo Ghadir inachukuliwa kuwa ni harakati ya kuunganisha Uislamu. Matukio mawili muhimu yalitokea wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukio la kwanza lilikuwa utume na tukio lililofuata lilikuwa ni ulezi na uimamu.

Kama kusingekuwa na Ghadir, dini Tukufu ya Uislamu ingeharibiwa, kwa sababu kama kusingekuwa na ufafanuzi, ubainishaji na maelezo ya Alawi (Yaani: Imam Ali a.s), dini ya Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ingeangamizwa kupitia Bani Umayya Bani Abbasi. Karbala pia iliambatana na Ghadir. Tunaamini kwamba mapinduzi yetu pia yako katika safu ya mawazo ya Ghadir na A'shura. Katika Siku ya Ghadir, mbali na kufanya sherehe za kuhuisha siku hii, umakini zaidi unapaswa kuonekana katika kutoa maudhui ya kiroho na kiakili.

Ayatullah Ramezani ameeleza kuwa itikadi mbili kuu za uliberali na ukomunisti zilikuwa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na akasema: Fikra za Kikomunisti zilitaka kuondoa kabisa dini, na fikra za kiliberali zilitaka kuweka mipaka ya dini.

Kabla ya Mapinduzi, walisema kuwa Mapinduzi ya kidini hayatatokea, lakini Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yalitokea na yalishinda. Kabla ya Mapinduzi, walikisema haiwezekani kuwepo kwa Mapinduzi ya Kiislamu, na wanachuoni hawakufikiri kwamba mabadiliko makubwa yangetokea nchini Iran, bali Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwepo na yalishinda, na hayo yalikuwa ni Mapinduzi yaliyoongozwa na Kiongozi Muadhamu, na kila kitu kuhusu Mapinduzi hayo kilikuwa ni ufunuo kwa dini, kwamba hayo si chochote ila ni muujiza na kazi ya Mwenyezi Mungu.

Uislamu, ujamaa na uongozi ni nguzo tatu za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, na kuendelea kwa Mapinduzi haya kunategemea kuhifadhi nguzo hizo. Adui anajaribu kupiga nguzo zote tatu za Mapinduzi. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yasingeshinda kwa mtazamo mdogo wa dini, Uislamu wenye rehema, na Uislamu wa kilimwengu. Bali, kilichofanya mapinduzi hayo kuwa na ushindi ni Uislamu mpana kwa mtazamo wa Imam Khomeini (RA). Uislamu ambao ulichukulia kumlilia Imam Hussein (RA) kuwa ni wa kisiasa.

Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yasingefanikiwa na kushinda kama yangekuwa na (mtazamo) maono finyu ya juu ya dini, Uislamu wenye huruma, na Uislamu wa kisekula. Bali, kilichopelekea ushindi wa Mapinduzi hayo ni Uislamu mpana kwa mtazamo wa Imam Khomeini (RA). Uislamu ambao ulichukulia kumlilia Imam Hussein (as) kuwa ni sehemu ya siasa safi ya Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha