Maadui
-
Baqaei: Lamerd Ni Alama ya Mapambano na Mateso ya Wairani Dhidi ya Maadui Wakubwa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema mji wa Lamerd ni ishara ya mapambano, mateso na dhamira ya wananchi wa Iran ya kukabiliana na maadui wakubwa, akisisitiza kuwa ziara yake mjini humo inalenga kuwashukuru wananchi na kukutana na familia za mashahidi.
-
IRGC: Mashambulizi ya Maadui Yanafanya Kufungwa kwa Mlango wa Hormuz Kuwa Imara Zaidi
IRGC imetangaza kuanza kwa majibu dhidi ya mashambulizi ya maadui, ikisema imefanikiwa kuangusha ndege ya kisasa isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 na kwamba upinzani wa wapiganaji wake katika Mlango wa Hormuz umevuruga mipango ya viongozi wa Marekani.
-
Naibu Mkuu wa Kisiasa wa IRGC kwa nchi za eneo: Ama muwafukuze Wamarekani au mpokee jibu kali
Naibu Mkuu wa Kisiasa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Jenerali Yadollahi Javani, amezitaka nchi za eneo hilo kuwaondoa wanajeshi wa Marekani na kurejesha udhibiti wa vituo vya kijeshi. Amesema iwapo nchi hizo hazitafanya hivyo, vikosi vya Iran vimeonyesha kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran kutoka eneo la Kuwait, Bahrain, Jordan au nchi nyingine litajibiwa kwa nguvu na kwa ukali.
-
Umoja wa Umma wa Kiislamu ndiyo njia ya kukabiliana na njama za maadui
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia nchini Lebanon, Sheikh Ali al-Khatib, amesema mshikamano wa Umma wa Kiislamu ni njia muhimu ya kukabiliana na njama za maadui, akisisitiza kuwa kusimama kwa Iran dhidi ya maadui zake kumetokana na umoja unaosisitizwa na Qur’ani.
-
Qalibaf: Tutawashinda Maadui katika Vita vya Kiuchumi kwa Kutegemea Uwezo wa Wananchi
Spika wa Majlis ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema Iran inakabiliwa na vita vya kiuchumi vya pande zote, akisisitiza kuwa nchi hiyo itawashinda maadui kwa kutegemea uwezo wa wananchi, sekta binafsi na taasisi mbalimbali za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Mkuu wa Jeshi la Iran: Jibu letu kwa vitisho vipya litakuwa la kuangamiza
Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Wanajeshi vya Iran, Meja Jenerali Ali Abdollahi, amesema Iran iko tayari kukabiliana na vitisho vipya, akisisitiza kuwa jibu la vikosi vya Iran litakuwa kali, pana na la kuangamiza.
-
Waziri wa Uchumi wa Iran: Ndoto ya maadui ya kuiangamiza uchumi wa Iran haitatimia
Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran, Ali Madani Zadeh, amesema maadui wa Iran hawatafanikiwa kuuharibu uchumi wa nchi hiyo, akidai kuwa wamekuwa wakiendesha vita vya mseto vinavyojumuisha mashambulizi ya kijeshi, mtandaoni na ya kiuchumi.
-
Jeshi la Iran: Hatima ya marubani watatu wa Su-24 bado haijajulikana
Msemaji wa Jeshi la Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Akrami Nia, amesema uchunguzi unaendelea kubaini hatima ya marubani watatu wa ndege za kivita aina ya Su-24 zilizoshiriki katika shambulio dhidi ya kambi ya Marekani ya Al Udeid, huku upande wa Qatar ukisema bado hauna taarifa kuhusu hali yao.
-
Rais Pezeshkian: Ustahimilivu wa Wairani ni Mfano wa Kupinga Uonevu na Ubeberu
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema ustahimilivu wa wananchi wa Iran ni mfano wa kipekee wa kupinga uonevu na ubeberu, huku akisisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia elimu, afya na huduma za kijamii.
-
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama Iran: Kuunga Mkono Marekani Kutawaletea Baadhi ya Watawala wa Eneo Hasara na Kushindwa
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama ya Iran, Hojjatul-Islam Gholam-Hossein Mohseni Ejei, amewatahadharisha watawala wanaoitegemea Marekani na kuamini ahadi za “Shetani Mkuu”, akisema kuwa hawatapata chochote isipokuwa hasara na kushindwa.
-
Kiongozi wa Iran: Ukiukaji wa Marekani unathibitisha saini yake haina thamani; Iran ina masomo yasiyosahaulika kwa adui
Katika ujumbe kuhusu kuaga kwa kishujaa kwa Kiongozi shahidi wa Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Mojtaba Khameni amesema kuwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Marekani wa makubaliano yaliyosainiwa kati ya marais wa Iran na Marekani umeonyesha tena kuwa saini ya rais wa Marekani haina thamani. Amesema pia kuwa Iran na mhimili wa muqawama wana masomo yasiyosahaulika kwa adui, kama ilivyoonekana kupitia ujasiri wa wapiganaji na uhodari wa wananchi wa maeneo ya kusini.
-
Ubalozi wa Iran Vienna: Iran Itaendelea Kusimama Imara na Kudumu Milele
Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Austria umesisitiza kuwa historia inaonyesha uimara wa wananchi wa Iran dhidi ya wavamizi, ukieleza kuwa maadui wa haki na wahalifu wanaotafutwa kimataifa hawatapata chochote isipokuwa fedheha na aibu.
-
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s): Iran Itaendelea Kuimarisha Uwezo Wake kwa Azma Kubwa Zaidi
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s), Meja Jenerali Ali Abdollahi, amesema Iran itaendelea kuimarisha uwezo wake wa ulinzi, usalama na maendeleo, akisisitiza kuwa taifa hilo halitayumba mbele ya vitisho na mashinikizo ya maadui wake.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Adui Aliishambulia Iran Akidhani Atashinda, Lakini Ameambulia Kushindwa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema kuwa mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Iran kwa uungaji mkono wa Marekani yalishindwa kufikia malengo yake kutokana na uimara, mshikamano na kujitolea kwa wananchi wa Iran, hali iliyowageuzia washambuliaji hasara na kushindwa.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kumtambua Imam Khomeini ni Taa ya Kuongoza Mustakabali wa Iran
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, amesema kuwa kuelewa na kumtambua Ruhollah Khomeini ni mwanga unaoongoza mustakabali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amebainisha kuwa kufuata mwenendo wa Ali ibn Abi Talib kumekuwa alama ya fahari kwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku akisisitiza kwamba taifa la Iran limesimama bega kwa bega na Muqawama na kuwa mfano wa kujivunia kwa mataifa yanayotafuta uhuru. Aidha, amewataka wananchi kudumisha umoja, busara na kuaminiana ili kuvuruga njama za maadui na kulinda mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Ghalibaf: Hatuamini Ahadi za Adui, Kipimo ni Matokeo ya Vitendo
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema kuwa Iran haitategemea ahadi za maadui katika medani ya diplomasia, akisisitiza kuwa mafanikio hupimwa kwa matokeo halisi na kwamba umoja wa wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha nafasi ya taifa hilo katika kukabiliana na mashinikizo ya nje.
-
Kaimu Waziri wa Ulinzi Iran: Taifa Limeshinda Kihistoria Dhidi ya Maadui Wake
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa wananchi wa Iran, kwa uungwaji mkono wa vikosi vya jeshi, wamefanikiwa kuwalazimisha maadui kupata “ushindi wa kihistoria”, akisisitiza pia umuhimu wa kuimarisha umoja wa Waislamu kupitia Eid al-Adha na msimu wa Hija.
-
Sepah: Njama za Adui Kuangusha Mfumo wa Uongozi wa Kiislamu Zashindwa kwa Busara ya Kiongozi Mkuu wa Iran na Uangalifu wa Wananchi
Jenerali Naeini amesema tangu 13 Juni 2025 adui alilenga kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran kwa kusababisha machafuko ya kijamii, lakini kwa busara ya Kiongozi Mkuu Sayyid Ali Khamenei (h.a.) na uangalifu wa wananchi, njama hizo zilivunjika. Pia katika ghasia za 8 Januari 2026 na operesheni ya “Ahadi ya Kweli”, juhudi za adui zilikabiliwa na kushindwa kabisa.
-
Jeshi la Sepah la Iran: Maadui Wameshindwa, Taifa Liko Imara
Jeshi la Mapambano la Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetaja kushindwa kwa maadui wa Iran katika miongo 47 iliyopita kama ishara ya nguvu, mshikamano wa taifa, na uangalifu wa wananchi. Taarifa hiyo pia inakumbusha changamoto za vikwazo na kipindi cha utegemezi, huku ikihimiza wananchi kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kitaifa ya 22 Bahman.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Mnamo tarehe 22 Bahman, kwa kuonesha dhamira na msimamo wenu thabiti, muwavunje moyo maadui
Kiongozi wa Mapinduzi amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman na kuonyesha utii kwa Jamhuri ya Kiislamu ni silaha muhimu ya kuwarudisha nyuma maadui wanaolenga Iran na maslahi ya taifa. Amefafanua kuwa nguvu ya taifa haitokani zaidi na makombora au ndege za kivita, bali inatokana na umoja, fikra, azma na msimamo thabiti wa wananchi.
-
Mwana wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Israel Aonyeshwa Kimakosa kama Aliyeuawa Iran
Vyombo vya habari vya maadui vimehusika katika kampeni ya upotoshaji dhidi ya Iran kwa kutumia picha za watu wasiokuwa na uhusiano na matukio ya ndani ya nchi hiyo. Hivi karibuni, hata picha ya mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kizayuni, Naftali Bennett, iliwasilishwa kimakosa kama mmoja wa waandamanaji waliodaiwa kuuawa, lengo likiwa ni kupotosha umma wa dunia na kuchochea hisia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Dhulfiqar: Kombora la Kivita la Iran Linaloashiria Makali ya Imam Ali (AS)
Israel tayari inatambua maana ya Dhulfiqar na imekwisha kuonja makali yake, huku Iran ikiwa imeapa kupigana na Israel vita vya mwisho endapo kutakuwa na shambulizi lolote toka kwa adui.
-
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi:
“Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimewapiga maadui zao Kofi lisilosahaulika”
Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.