Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ali Lariyani, Mshauri Mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa suala la kuanza mazungumzo kwa sasa halipo mezani, akisisitiza kuwa: “Mpinzani wetu ameanzisha vita dhidi yetu. Hatua ya kwanza ni aeleze ni kwa nini walitushambulia.”
Akiwa na msimamo thabiti, Lariyani alionya dhidi ya haraka katika suala la mazungumzo, akieleza kuwa: “Mazungumzo ni mbinu tu ya kisiasa (Taktiki), na si lengo lenyewe.”
Aliongeza kuwa ni juu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuamua ni lini na wapi mbinu hiyo itumike: “Muachieni Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi aamue ni wakati gani na wapi ni sahihi kutumia mbinu hii.”
Your Comment