13 Aprili 2025 - 15:50
Adui amechanganyikiwa na ana hofu kuhusu maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu / Kudumisha utayari wa hali ya juu na uboreshaji wa maunzi na programu

Ayatullah Khamenei amehusisha hasira za watu wasio na mapenzi mema (wenye nia mbaya) na mabishano yao kwenye vyombo vyao vya habari kuwa ni kuzidisha maendeleo ya Iran na kusema: "Wanabainisha mambo (matakwa) ambayo ni sehemu ya matamanio yao kwa anuani kuwa ni habari na uhakika, na ni lazima kubuni njia za kukabiliana na dhana na propaganda hizi."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (A.S) - ABNA - Alasiri ya leo katika kikao na kundi la makamanda na maafisa wa jeshi kwa mnasaba wa kuukaribisha Mwaka Mpya, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amevitaja vikosi hivyo kuwa ni uzio wa nchi na kimbilio la Taifa dhidi ya mvamizi yeyote yule. Akisisitiza kuendelea kuimarishwa kwa utayari wa hali ya juu na tahadhari za vifaa na programu mbalimbali ili kutimiza jukumu hili la kitaifa, alisema: "Maendeleo ya nchi yamewakasirisha na kuwakatisha tamaa watu wenye nia mbaya na wasio na mapenzi mema na Iran."

Katika kikao hiki, Ayatollah Khamenei ameelezea utayarifu wa zana za kijeshi za majeshi ya Iran kuwa ni kuimarisha uwezo wao wa silaha na kuboresha uwezo wao wa taasisi za kijeshi na mashirika, na maisha na akaongeza: "Pamoja na utayari wa vifaa vya kijeshi, na utayari wa programu, maana yake ni hii kwamba imani katika lengo na dhamira ya mtu na uhakika wa uhalali wa njia, ni jambo muhimu sana, na kuna juhudi za kiuadui za kulipotosha hilo."

Adui amechanganyikiwa na ana hofu kuhusu maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu / Kudumisha utayari wa hali ya juu na uboreshaji wa maunzi na programu

Ameuona uwepo wa Kiislamu na wa kujitegemea wa mfumo wa Kiislamu kuwa ni sababu ya kuchochea uadui dhidi yake, na akaongeza: “Kinachomfanya adui kuwa na hisia kali si jina la Jamhuri ya Kiislamu, bali ni mapenzi ya nchi zingine kuwa za Kiislamu, zenye kujitegemea, na zenye utambulisho wake, na kutowategemea wengine kwa ajili ya hadhi yake, jambo ambalo linawafanya wakasirike mno.

Akirejelea mfano wa mielekeo miwili ya wanyanyasaji wa kimataifa katika kujiruhusu kuwa na aina kali zaidi za silaha na kutowaruhusu wengine kufanya maendeleo ya ulinzi wa kijeshi, Kiongozi wa Mapinduzi alisema: "Hakika, imani, utashi, ujasiri, na kumtumaini Mwenyezi Mungu lazima viwepo kwa kiwango cha juu kabisa katika jeshi, kwa sababu majeshi ya fahari na makubwa ambayo hayajaweza kuwa na sifa hizi katika historia, yameshindwa."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha