Ayatollah Khamenei amesisitiza kuwa, Wamarekani wanapaswa kujua kwamba kamwe hawatafika popote kwa vitisho dhidi ya Iran na akasema: Wao na wengine wanapaswa kujua kwamba iwapo watafanya jambo lolote ovu kwa Taifa la Iran, watapigwa kofi kali.
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa mwanzo wa mwaka mpya wa 1404 Hijria Shamsia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya kuwa ni mwaka wa "Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji".