Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (as) -ABNA-Mchana wa leo, Ayatollah Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, atatoa ujumbe wake wa pili kupitia televisheni kwa taifa la Iran kufuatia hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
Katika ujumbe wake wa kwanza, aliwasifu wananchi wa Iran kwa mwenendo wao wa utulivu, ujasiri na umahiri kwa wakati huu waliouonesha katika tukio hilo la hujuma ya kijinga na ya kinyama kutoka kwa adui Mzayuni.
Alisema kwamba tabia hiyo ni ishara ya ukomavu wa taifa hilo na uimarishaji wa akili na kiroho.
Kiongozi huyo alisisitiza kuwa: "Wananchi wa Iran wamesimama imara dhidi ya vita vya kulazimishwa, na vilevile wamesimama imara dhidi ya amani ya kulazimishwa; taifa hili halitakubali kulazimishwa na mtu yeyote."
Pia, alipokuwa akizungumzia matamshi ya vitisho na ya kejeli yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Ayatollah Khamenei alisema: “Watu wenye busara wanaoijua Iran, watu wake na historia yake, hawazungumzi na taifa hili kwa lugha ya vitisho, kwa sababu taifa la Iran halisalimu amri kamwe.
Wamarekani wanapaswa kufahamu kuwa aina yoyote ya uvamizi wa kijeshi kutoka kwao hakika itasababisha madhara yasiyoweza kufidiwa.”
Your Comment