Ujumbe
-
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC): Tukivamiwa, tutawasha moto wa Jahannam dhidi ya wavamizi
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Pakpour, katika mazungumzo na Qasim al-A’araji, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq, amesema kuwa: “Katika vita vya siku 12, tulishambulia kwa nguvu na usahihi mkubwa na tuliharibu malengo yote yaliyolengwa.”
-
Scott Ritter: Iran Yailazimisha Israel Kusitisha Vita vya Siku 12 kwa Teknolojia ya Juu ya Makombora
Aliyekuwa askari wa Kikosi cha Wanamaji cha Marekani na mpelelezi wa zamani wa Umoja wa Mataifa kuhusu silaha za maangamizi, Scott Ritter, amesema kuwa Iran katika vita vya siku 12 haikurudisha tu udhibiti wa hali ya vita, bali pia iliadhibu vikali utawala wa Kizayuni kwa kutumia teknolojia yake ya kisasa ya makombora ya masafa marefu.
-
Iran yashuku ujumbe wa Netanyahu kuhusu kutoshambulia tena
"Vikosi vya ulinzi vya Iran vipo katika hali ya tahadhari ya juu kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa hila kutoka Israel, na hatuamini nia hizi".
-
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Kamanda Bahman Kargar kufuatia kifo cha Kamanda Alireza Afshar
Mkuu wa Taasisi ya Kuhifadhi na Kueneza Thamani za Ulinzi Mtakatifu na Mapambano ametoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kifo cha Kamanda wa IRGC, Brigedia Sardar Alireza Afshar.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala
Ayatollah Khamenei katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala alielezea mambo muhimu yanayohusu mkutano huu pamoja na sifa za sala.
-
Sheikh Ali Salman kutoka gerezani: “Kama ningekuwa huru, ningetamani kuwa pamoja na wapigania uhuru wa ‘Msafara wa Ustahimilivu (Sumud)msafara”
“Kile mnachokifanya katika msafara huu kinaheshimiwa katika dini zote, sheria zote na mila zote; ni ushahidi kuwa dhamiri ya kibinadamu bado haijafa. Harakati yenu ni fahari kwa wote sisi.”
-
Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Ayatollah Sistani kufuatia Kifo cha Mke Wake
Kufuatia kifo cha mke wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, alituma ujumbe wa rambirambi kwa Marja’ huyu mkubwa.
-
Meja Jenerali Musawi: Jeshi la Ukombozi litatoa jibu lililo juu ya fikra za waonevu (waovu)
Rais wa Makao Makuu ya Majeshi ya Ulinzi wa Iran amesema: Tunawapa uhakika wananchi wa Iran wenye heshima na ushujaa kuwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutegemea uwezo wao, ubunifu na mshangao wa kimkakati, viko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya madhalimu na waonevu wa dunia kwa majibu ya wakati muafaka, makali, ya kujutia na yaliyo zaidi ya fikra zao.
-
Mkuu wa Majeshi: Vikosi vya Ulinzi vya Iran Vitatoa Jibu Kali Zaidi ya Mawazo ya Wavamizi
“Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa mwongozo wa Kiongozi Muadhamu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde), vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko tayari kugeuza tishio lolote kuwa fursa ya kustawisha nguvu za taifa na kuinua hadhi ya Iran katika mizani ya kimkakati ya kikanda na kimataifa. Jibu letu kwa maadui litakuwa la wakati, kali, la kuumiza na zaidi ya walivyowahi kufikiria.”
-
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) kufuatia kifo cha Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi
Kufuatia kifo cha Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi, mkuu wa ofisi ya masuala ya kifedha ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) alitoa ujumbe wa rambirambi.
-
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Faqihi kwa mnasaba wa kufariki kwa Ayatollah Mousavi Yazdi
Ayatollah Mohsen Faqihi ametuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Mali (Wujuhat) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
-
Kuhalalisha Uhusiano na Israel ni Usaliti wa Wazi na Msaada wa Moja kwa Moja kwa Adui" – Ayatollah Isa Qassim
Ayatollah Qassim amegusia pia matamshi ya karibuni ya Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, pamoja na vita vya kinyama anavyoendeleza kwa msaada wa kimkakati kutoka Marekani.
-
Kiongozi wa Mapinduzi Aomboleza Kifo cha Hujjatul-Islam Naeim Abadi
Mheshimiwa Ayatollah Khamenei ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanazuoni mpiganiaji, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholamali Naeim Abadi.
-
Ujumbe wa Shukrani kutoka kwa Ayatollah Faqihi kwa Taifa Tukufu la Iraq
“Nyinyi mmekuwa wenyeji bora na waagizaji bora kwa mahujaji wa Arubaini.”
-
Ujumbe wa Rambirambi wa Ayatollah Husseini Bushehri Kufuatia Kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian
Rais wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian.
-
Beirut - Wananchi wa Lebanon Wamiminika Mitaani Kuiunga Mkono Hizbullah na Mapambano ya Muqawama
Wakisambaza ujumbe wao kwa sauti na maandamano, wananchi hao wamesisitiza kuwa Hizbullah si tu harakati ya kijeshi, bali pia ni nguzo muhimu ya taifa katika ulinzi wa mipaka na heshima ya Lebanon. Kwao, wazo la kuondoa silaha za harakati hiyo ni sawa na kuiweka Lebanon mikononi mwa maadui wake.
-
"Watu wenye busara wanaoijua Iran,watu wake na historia yake,hawazungumzi na taifa hili kwa lugha ya vitisho,kwa sababu taifa la Iran halisalimu amri"
"Wamarekani wanapaswa kufahamu kuwa aina yoyote ya uvamizi wa kijeshi kutoka kwao hakika itasababisha madhara yasiyoweza kufidiwa.”
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia tukio la moto katika Bandari ya Shahid Rajaei, Bandar Abbas
Ayatollah Khamenei amewaombea Marehemu rehma na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na amewatakia familia za wahanga subira na utulivu wa moyo. Vilevile, amewaombea majeruhi wapate uponyaji wa haraka.
-
Ujumbe wa Ayatollah Ramezani wa rambirambi kwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Ukaribu wa Madhehebu za Kiislamu
Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) ametoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Baba yake Hojat al-Islam Wal-Muslimin, Dakta Hamid Shahriari.