Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Idara ya Utamaduni na Itikadi: Ayatollah Sheikh Isa Qassim, Mwanazuoni mkubwa kutoka Bahrain, ameonya kupitia tamko maalum kuwa harakati ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, iwe hadharani au kwa njia ya siri, si jambo la maelewano ya mapema tu, bali ni msaada wa kweli kwa adui na ushiriki wa moja kwa moja katika njama zake za kuidhoofisha na kuiangamiza Ummah wa Kiislamu.
Amesisitiza kuwa mwenendo huu wa kuwa karibu na utawala wa Kizayuni ni usaliti wa hali ya juu, unaoashiria kutengana kwa mtu na Ummah, dini yake, maadili, heshima ya kiutu, na hisia za wivu wa kidini.
Ayatollah Qassim amegusia pia matamshi ya karibuni ya Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, pamoja na vita vya kinyama anavyoendeleza kwa msaada wa kimkakati kutoka Marekani, na kueleza kuwa:
“Ujumbe wa vita hii unalenga waziwazi Ummah wa Kiarabu na Kiislamu, kwa nia ya kuwaweka chini ya udhibiti kamili wa Israeli – iwe katika hali ya vita au amani. Udhibiti huu unatekelezwa chini ya ndoto ya uongo ya ‘Israeli Kubwa’ kama ilivyotajwa kwenye Taurati yao ya bandia, na mipaka yake inapita hata mipaka ya kijiografia.”
Ameongeza kuwa:
"Vita hii tayari imeanza, na madhara yake yanakusudia kugusa kila nchi ya Kiarabu na Kiislamu, pamoja na kila kiongozi anayesimama kwa uaminifu kwa ajili ya watu wake."
Katika hitimisho lake, Ayatollah Isa Qassim alimuomba Mwenyezi Mungu aunganishe Ummah wa Kiislamu katika njia ya jihadi kwa ajili ya kulinda dini yao, ardhi yao, na maslahi yao. Pia ameomba ushindi na heshima ya wazi kutekelezwa kwa Ummah huu wa Kiislamu.
Your Comment