Ayatollah Qassim amegusia pia matamshi ya karibuni ya Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, pamoja na vita vya kinyama anavyoendeleza kwa msaada wa kimkakati kutoka Marekani.
Tunafundishwa Dua hii:
اللَّهُمَّ اجْبُرْ كَسْرَ قَلْبِي، وَصَبِّرْنِي عَلَى مَا فَاتَنِي...
"Ewe Mwenyezi Mungu! Tibu moyo wangu uliovunjika, nivumilishe juu ya kilichonipita..."
Kwa Dua hii unajielekeza kwa Allah (SWT) kama Mponyaji wa nyoyo zilizovunjika na Mtulizaji wa roho zilizochoka. Inafundisha kumkabidhi Allah maumivu ya moyo, kukubali kuwa si kila tulichokitaka ni chema kwetu, na kumuomba Atuchagulie kilicho bora.