Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA -; Ayatollah "Reza Ramezani", Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s), katika ujumbe wake, alitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Baba wa Hojat al-Islam Wal-Muslimin, Dakta Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu.
Nakala ya ujumbe huu ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Hojjat al-Islam wal-Muslimin, Mheshimiwa Dkt. Hamid Shahriari (zidumu taufiq zake).
Habari za huzuni na kusikitisha za kifo cha Baba yako; zimetufikia.
Nina matumaini madhubuti kwamba Marehemu huyu, alikiishi kwa imani na matendo mema, na atakuwa chini ya neema na rehma za Mwenyezi Mungu na uombezi wa Maasumina (amani iwe juu yao), na atafufuliwa pamoja na Mawalii wa Mwenyezi Mungu.
Kwa minajili hiyo, ninatoa pole kwako Mheshimiwa na familia yako kutokana na msiba huu, na ninawaombea subira na malipo mema ya Mwenyezi Mungu waliobakia (katika familia yake).
Hakika Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.
Your Comment