Madhehebu
-
Ayatollah Ashrafi Shahroudi alipokutana na viongozi wa Shirika la Habari la “Abna” alisema:
"Kuonyesha huruma na kujali kwa ajili ya mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s) huleta maendeleo katika kazi mbalimbali"
"Kwa juhudi za Imam na Mapinduzi, jina la Ahlul Bayt (a.s) limejulikana na kutambulika kote duniani. Sababu kuu ya uadui wote wa naadui dhidi ya IRAN, unatokana na IRAN na Jamhuri ya Kiislamu kuzingatia na kufuatilia zaidi mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s). Kuanzia vita vya miaka minane hadi fitina ya Daesh na hata uvamizi huu wa utawala wa Kizayuni ni kwa sababu ya imani ya dhati ya Taifa la Iran na uvumilivu wa Mashia."
-
Msimamo Mkali wa Hizbullah Dhidi ya Jaribio la Kuvunjwa kwa Silaha za Muqawama: Azimio Jipya la Serikali ya Nawaf Salam ni Tishio kwa Uhuru wa Lebanon
Chama cha Hizbullah kimetoa tamko kali kupinga uamuzi mpya wa serikali inayoongozwa na Nawaf Salam, ambao wanauona kama hatua ya hatari ya kudhoofisha muqawama (mapambano ya ukombozi) na kukabidhi usalama wa Lebanon kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika taarifa hiyo, Hizbullah imesisitiza kuwa itakabiliana na uamuzi huu kwa msimamo thabiti kama hatua isiyokubalika kabisa, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda silaha za kujihami na kuimarisha jeshi la taifa kwa ajili ya kutetea ardhi na uhuru wa Lebanon. Lebanon Bado Chini ya Vitisho vya Israel na Marekani
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu: "Uhalifu wa Israel ni Jeraha kwenye Mwili wa Umma wa Kiislamu"
Hojjatul Islam Wal-Muslimeen Dakta Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu ameandika katika ujumbe wake kwenye Twitter yake kuwa: "Uhalifu wa Israel sio tu kuishambulia Iran, bali pia ni jeraha kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu."
-
Saumu ya Arafa | Kwa Mujibu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari: "Kufunga Siku ya Arafa ni Sunna na si wajibu"
Hoja na Dalili Juu ya Sunna ya Saumu ya Siku ya Arafa: Riwaya kadhaa za Kishia zinaelezea fadhila za kufunga Siku ya Arafa, kama vile riwaya ya Abdur_Rahman bin Abi Abdillah kutoka kwa Abul Hassan (as).
-
Majlis ya Mazazi ya Imam Ridha (as) yafanyika Jamiat Al-Mustafa(s), Tanzania | Hadithi Toka Vyanzo vya Kisunni Zinathibitisha Makhalifa Kumi na Wawili
Lengo la Mazungumzo Haya ni: Kuleta maelewano baina ya Madhehebu za Kiislamu na kuonyesha kuwa msingi wa Uimamu na Ukhalifa wa Maimam Kumi na Wawili wa Ahlul-Bayt (a.s), wanaofuatwa na Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, una mizizi pia katika vyanzo vinavyokubalika vya Kisunni.
-
Katika kongamano la Kimataifa la "Sayansi, Dini, na Akili Bandia" lililofanyika Zagreb, Shahriyari:
Akili bandia si dhana bali ni mshirika kwa Binadamu katika kila dakika ya maisha yake
Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Kuleta Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu alisema: Mjadala wa akili bandia ni mpana sana na unahusisha kila nyanja ya maisha ya binadamu, na kila mtu anapaswa kuuhusisha kulingana na wajibu wake mwenyewe.
-
Tarehe 25 Shawwal Mwaka 148 Hijiria, ulimwengu wa Kiislamu ulipatwa na Huzuni kufuatia kuondokewa na mmoja wa Ahlul-Bayti wa Mtume wa Uislamu (saww)
Licha ya kwamba Ahlul-Bayti wa Mtume (s.a.w.w) walikabiliwa na changamoto tofauti kisiasa na kijamii, lakini walijitahidi kuhakikisha wanainua bendera ya dini ya Kiislamu katika zama zao zote. Dakta Shahid Mutwahhari, mwanafikra mashuhuri wa Iran anaandika kwa kusema: " Ahlul-Bayti (a.s) walikuwa wakichunga maslahi ya Kiislamu na Waislamu kwa ujumla".
-
Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!
Wakati picha za kutisha za mauaji ya halaiki huko Gaza zimeamsha dhamiri za wanadamu kote ulimwenguni, ukimya mzito katika baadhi ya jamii za Kiislamu, haswa kati ya duru za kidini, unatia shaka. Kwa nini baadhi ya watu wanauita Upinzani (Muqawamah) huu "wa Kidini" au "Kisiasa" na kuondoa uungaji mkono wao wakati Hamas, Hezbollah, au Iran inaposimama dhidi ya Israel?!, Je, (kupinga) dhulma na ukandamizaji kwa Wapalestina unahitaji idhini ya Madhehebu?
-
Ujumbe wa Ayatollah Ramezani wa rambirambi kwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Ukaribu wa Madhehebu za Kiislamu
Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) ametoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Baba yake Hojat al-Islam Wal-Muslimin, Dakta Hamid Shahriari.