20 Aprili 2025 - 19:32
Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Wakati picha za kutisha za mauaji ya halaiki huko Gaza zimeamsha dhamiri za wanadamu kote ulimwenguni, ukimya mzito katika baadhi ya jamii za Kiislamu, haswa kati ya duru za kidini, unatia shaka. Kwa nini baadhi ya watu wanauita Upinzani (Muqawamah) huu "wa Kidini" au "Kisiasa" na kuondoa uungaji mkono wao wakati Hamas, Hezbollah, au Iran inaposimama dhidi ya Israel?!, Je, (kupinga) dhulma na ukandamizaji kwa Wapalestina unahitaji idhini ya Madhehebu?

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (A.S) - ABNA - Hojjatul Islam Syed Jawad Naqvi, Mkuu wa Harakati ya Mwamko ya Umma wa Mustafa nchini Pakistan, alisisitiza katika andiko lake akisema: Ikiwa nchi ya Kisunni itaiunga mkono Palestina kijeshi wazi wazi na hadharani, je, uungaji mkono huu unachukuliwa kuwa ni "Halali", lakini ikiwa Iran itafanya vivyo hivyo, je, ghafla hali itabadilika na kuwa "Ajenda ya Madhehebu"?!.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Sehemu kamili ya Nakala ya andiko lake ni kama ifuatavyo:

Uhalifu na mauaji ya kimbari huko Gaza yametikisa dhamiri za walimwengu, lakini inashangaza kwamba katika nchi kama Pakistan, hata kati ya nchi za kimadhehebu, kuna kimya cha kushangaza na kizito. Ukimya ambao sio wa muda tu, bali ni taswira ya kudumaa kifikra na mifarakano ya kimazungumzo ambayo, badala ya kuamsha dhamiri ya pamoja ya Ummah wa Kiislamu, imenasa katika chuki za kimadhehebu na kijiografia!.

Ukandamizaji wa Wapalestina haukomei (na kuishia) kwa tukio au wakati maalum. Kwa miezi kadhaa sasa, miili ya mashahidi, hospitali zilizoharibiwa, watoto yatima, baba na mama waliojeruhiwa, na vitongoji vilivyochomwa moto vimekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watu wa Gaza.

Kwa hivyo swali ni hili: Kwa nini ghafla hisia zinazoumiza na fatwa zinatolewa kwa sasa?. 

Ikiwa hisia hizi ni za kweli kwa watu wa Palestina, kwa nini hazikutajwa katika nyakati ambazo Hezbollah, Hamas, na Iran zilisimama kupinga uvamizi wa Israeli?!.

Wakati huo, duru nyingi za kidini na kimadhehebu zilikaa kimya. Uhalali wa ukimya huu ulikuwa kwamba "suala hili linahusiana na Iran" au "ni sehemu ya siasa zinazoegemea zaidi kwa Shia." Mtazamo huu uliuweka Muqawama (Upinzani) wa Palestina ndani ya mifumo ya kimadhehebu, na kulifanya kuwa moja ya masuala muhimu na matakatifu ya Umma wa Kiislamu kwa kuigeuza Palestina kuwa mhanga wa masimulizi yenye mgawanyiko. 

Ukimya huu si wa bahati mbaya; Bali, ni matokeo ya propaganda zilizokokotwa, zenye lengo la kuendeleza mgawanyiko wa kimadhehebu ndani ya Ummah wa Kiislamu. Wakati huo vuguvugu la upinzani (la Palestina) linachukuliwa kuwa mtuhumiwa kwa sababu tu linaungwa mkono na nchi fulani au madhehebu fulani, hali hii kwa hakika inaimarisha na kutia nguvu masimulizi ya dhalimu.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Ikiwa nchi ya Kisunni inaiunga (au itaiunga) mkono Palestina kijeshi waziwazi na hadharani, je, msaada huo unachukuliwa (au utachukuliwa) kuwa ni "Halali", lakini ikiwa Iran itafanya vivyo hivyo, je, ghafla hali itageuka na kuwa "Ajenda ya Madhehebu"?!

Je, tuna haki ya kuchukua msimamo dhidi ya uonevu ikiwa tu msimamo huo unapatana na utambulisho wetu wa kimadhehebu?. Njia hii ya kufikiri ni hatari sana. Na sio tu kwamba inapunguza uungwaji mkono kwa watu wa Palestina, bali pia inasukuma Ummah wa Kiislamu kuwa mbali kabisa na misingi kuelekea utambulisho. Ikiwa kweli suala la Palestina ni suala la Ummah wa Kiislamu, basi uungaji mkono wake unapaswa kumjumuisha kila mtu, serikali, au kikundi ambacho kinasimama kwa dhati na wanyonge, bila kujali asili yao ya kisiasa au kimadhehebu.

Ukweli ni huu kwamba Iran, licha ya kuwa na misingi yake ya kisiasa na kimadhehebu, imekuwa miongoni mwa waungaji mkono watiifu na wa dhati wa Muqawama (Upinzani) wa kijeshi wa Palestina unaopigania Haki na ardhi za Wapalestina. Tukikataa kuungwa mkono na nchi hiyo kwa sababu tu ni nchi ya Kishia, hii itakuwa ni kinyume na haki na mantiki (akili) salama. Mtazamo huo sio tu kwamba una madhara kwa Wapalestina, bali pia unadhoofisha Umoja wa ulimwengu wa Kiislamu.

Kuunga mkono upinzani wa Palestina ni jukumu la kanuni na misingi ya kiislamu, ambalo halipaswi kuwekewa masharti na nani anayesimama katika njia yake. Wakati Iran au makundi washirika wake kama vile Hezbollah au Hamas yanapoingia kwenye vita, kigezo chetu cha kuungwa mkono au upinzani kisiwe ni itikadi tu, bali kigezo kiwe ni je, hawa wanasimama na wanaodhulumiwa au la.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Mgawanyiko wa kimadhehebu hauidhuru Palestina tu, bali pia unaharibu umoja wa Ummah wa Kiislamu. Tukikubali au kukataa upinzani (dhidi ya batili na udhalimu wa uzayuni) kwa kutegemea na kutizama kuwa ni nani anayeuongoza, basi kwa hakika tunaelekea katika kuchagua kwenye suala la haki. Hii ina maana kwamba tunahukumu kanuni, haki, na uungaji mkono kwa wanaokandamizwa kulingana na watu binafsi, nchi na madhehebu.

Maandamano yatakuzwa tu wakati picha za kuhuzunisha moyo zitachapishwa kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya habari vya Kiarabu vitalazimika kuakisi ukweli. Lakini upinzani unapoendelea kwenye uwanja wa vita, wakati damu yao inatiririka, na adui anajibu kwa kufanya mauaji ya halaiki, na sisi tunanyamaza na kukaa kimya, au tunaishia kusema na kuiita kuwa hii ni ajenda ya Iran hivyo tuikatae, tutakuwa hatuikomoi Iran, bali tunawakomoa Waislamu wa Palestina wanaodhulumiwa na kukandamizwa.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Fikra hiyo pia ni aina ya utumwa wa kiakili. Mtego wa kiakili ambao umeukumba Umma wa Kiislamu kiasi cha kutoegemea upande wowote na wakati mwingine hata kupinga vita vyake..

Sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote, ni muhimu kwa Umma wa Kiislamu kutolitazama suala la Palestina kwa mitazamo ya kimadhehebu au ya kijiografia. Palestina ni suala la kibinadamu, maadili na kanuni (misingi ya Kiislamu). Yeyote, bila kujali dini au dhehebu, au utaifa, anastahili kuungwa mkono ikiwa anasimama kwa uaminifu na waliodhulumiwa.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Kama vile Uislamu haukomei kwa rangi, kabila, au lugha maalum, msaada kwa wanaodhulumiwa na kukandamizwa haupaswi kuwa na mipaka ya Madhehebu. Ikiwa tutakataa msimamo wa nchi au kikundi kwa msingi wa utambulisho wake wa kimadhehebu tu, basi kwa hakika, sisi wenyewe tutakuwa tunaanguka katika chuki ile ile ambayo Uislamu umetuonya dhidi yake.

Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!

Bendera ya Palestina isiwe tu kisingizio cha mihemko ya muda mfupi au maandamano ya kitambo tu, bali inapaswa kuwa ishara ya msimamo wenye kanuni, uhuru wa kiakili na umoja wa Umma wa Kiislamu. Bendera hii haipaswi kuhusishwa na ajenda, wakala, au dhehebu lolote mahususi, bali inapaswa kuzingatiwa kuwa ishara ya upinzani dhidi ya dhulma na ukandamizaji na ushindi wa ukweli.

Ikiwa Umma wa Kiislamu hautaelewa na kutambua kanuni hii ya msingi ya Kiislamu, basi kwa hakika hauwezi kamwe kuitendea Haki Palestina wala Umma wenyewe kujitendea Haki.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha