Makazi
-
Hamas: Kuanguka kwa Jengo la Al-Saada ni Sura Mpya ya Vita vya Mauaji ya Kimbari Gaza
Harakati ya Hamas leo Jumatano imeitaja Israel kuwa inawajibika kwa kuanguka kwa Jengo la Al-Saada juu ya wakazi na watu waliokimbia makazi yao katika Jiji la Gaza. Hamas imeeleza tukio hilo kuwa ni sura mpya ya madhara makubwa ya kibinadamu yanayotokana na vita dhidi ya Ukanda wa Gaza. Tangu alfajiri ya leo, timu za uokoaji za Palestina zimefanikiwa kutoa miili ya mashahidi 20 kutoka chini ya vifusi, wakiwemo watoto 6, huku watu wengine kadhaa wakiendelea kutafutwa na kutajwa kuwa hawajulikani walipo.
-
Iran Yaelekeza Ujumbe kwa Baraza la Usalama la UN Kufuatia Mashambulizi Mapya ya Marekani na Shambulio kwenye Sherehe ya Harusi
Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Gholam Hossein Darzi, amelaani mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran, likiwemo shambulio kwenye nyumba ya makazi iliyokuwa ikiandaliwa sherehe ya harusi, akisema tukio hilo ni mfano wa uhalifu wa kivita.
-
IRGC yatangaza awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2"; yadokeza kushambulia vituo vya mawasiliano na makazi ya wanajeshi wa Marekani Bahrain
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa katika awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2" lililenga maghala ya silaha, kituo cha mawasiliano ya satelaiti na jengo la makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kambi ya Al-Juffair nchini Bahrain.
-
Mkuu wa Mahakama ya Iran: Adui Amepiga Magoti Mbele ya Iran Licha ya Uwezo Wake Wote
Mkuu wa Mahakama ya Iran amesema njama za maadui za kuisambaratisha Iran zimeshindwa, akisisitiza kuwa uimara wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na mshikamano wa wananchi umezuia machafuko na kuimarisha nafasi ya Iran duniani.
-
Ukraine Yashambulia Makaazi ya Putin kwa Ndege Droni 91 / Trump Ashtuka
Ikulu ya Kremlin jioni ya Jumatatu ilitangaza kuwepo kwa mawasiliano ya simu kati ya marais wa Urusi na Marekani, na kubainisha kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, alishtushwa na shambulio la ndege zisizo na rubani (droni) la Ukraine dhidi ya makaazi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
-
Baridi Kali ya Hewa Gaza Yachukua Maisha ya Mtoto Mchanga
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa kurekodiwa kwa kisa hiki, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na baridi kali na athari za mfumo huo wa hali ya hewa, baada ya kuhamishiwa katika hospitali za Gaza, imefikia watu 13.
-
UMOJA WA MATAIFA: Nusu ya Wakazi wa Afghanistan Wanahitaji Msaada wa Kibinadamu
Ofisi ya Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa mwaka 2026 takribani watu milioni 22 — sawa na asilimia 45 ya watu wa Afghanistan — watahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu; huku idadi ya watu wenye uhaba mkali wa chakula ikifikia milioni 17.4 na milioni 5.2 wakiwa katika hatari ya njaa kali.