16 Juni 2025 - 15:41
Baqaei: Kushambulia hospitali ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhalifu wa kivita

Akilaani shambulio la kombora la utawala haramu wa Kizayuni katika Hospitali na Kituo cha Tiba cha Farabi huko Kermanshah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ameandika: "Mashambulizi dhidi ya hospitali pamoja na mashambulizi katika maeneo ya makazi ya watu ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na jinai ya kivita."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as)-ABNA-, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni amelaani shambulio la kombora la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Hospitali na Kituo cha Tiba cha Farabi huko Kermanshah na kuandika: "Mashambulizi dhidi ya hospitali pamoja na mashambulizi katika maeneo ya makazi ya watu ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhalifu wa kivita."

Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ameandika katika akaunti yake ya X: Jinai nyingine ya utawala ghasibu wa Israel: Hospitali ya Farabi katika mji wa Kermanshah magharibi mwa Iran ilikuwa shabaha ya mashambulizi ya kichokozi ya utawala wa Israel; kushambulia hospitali pamoja na kushambulia maeneo ya makazi ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhalifu wa kivita; lakini haya ni maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa serikali: Mashambulizi kwenye maeneo ya makazi! Historia itawahukumu vikali wafuasi na wanaohalalisha utawala huu wa kichokozi na wa mauaji ya halaiki.

Inafaa kuashiria kuwa, mwendo wa saa tisa alfajiri ya kuamkia leo, utawala haramu wa Kizayuni ulifanya shambulio la kombora katika Hospitali na Kituo cha Tiba cha Farabi na majengo ya jirani. Kufuatia shambulizi hili, Hospitali ya Farabi imepata madhara makubwa sehemu mbalimbali. Vikosi vya uokoaji vimetumwa mara moja kwenye eneo la tukio na uchunguzi na shughuli za uokoaji zinaendelea.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha