Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza utayari wa nchi yake kwa ajili ya kukomesha ugaidi na kuimarisha usalama wa mipaka ya Iran na Pakistan.
Akilaani shambulio la kombora la utawala haramu wa Kizayuni katika Hospitali na Kituo cha Tiba cha Farabi huko Kermanshah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ameandika: "Mashambulizi dhidi ya hospitali pamoja na mashambulizi katika maeneo ya makazi ya watu ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na jinai ya kivita."