Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Vyanzo vya Palestina vilitangaza kwamba mashahidi 15 walihamishiwa katika Hospitali ya al-Ma'amedani kutokana na shambulio la bomu kwenye jengo la makazi kwenye Mtaa wa al-Mansoura ulioko katika kitongoji cha Shujaiyeh katika Jiji la Gaza, na idadi kadhaa ya mashahidi bado wako chini ya vifusi.
Kwa upande mwingine, mizinga ya Israel ilishambulia kwa nguvu kubwa kusini mwa Gaza. Jeshi la Israel liliteketeza nyumba moja katika eneo la Qizan al-Najjar, Kusini mwa Mji wa Khan Yunis, Kusini mwa Gaza. Katika matokeo ya shambulio hili, mtu mmoja aliuawa.
Duru za Wapalestina zimeripoti kuuawa Shahidi kwa Wapalestina wasiopungua 24 katika mashambulizi ya anga ya asubuhi huko Gaza.
Boti za kivita za utawala wa Kizayuni zilifyatua risasi chini ya maeneo ya Pwani ya Mji wa Khan Yunis.
Eneo la Tal al-Stan Magharibi mwa Mji wa Rafah pia liko chini ya moto wa mizinga ya utawala wa Kizayuni na vifaru vya Israel navyo vinarusha risasi katika eneo hilo.
Eneo la Al-Yarmuk lililo katikati mwa Ghaza halijaepushwa na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni. Maeneo ya Mashariki ya kambi ya al-Brij katikati mwa Gaza pia yalishambuliwa na mizinga ya Israel.
Utawala wa Kizayuni pia ulifanya mashambulizi matatu ya anga katika mji wa Absan al-Kabirah ulioko Mashariki mwa Khan Yunis Kusini mwa Gaza.
Helikopta ya utawala wa Kizayuni pia iliwafyatulia risasi wakazi wa Mji wa Rafah ulioko Kusini mwa Gaza.
Wakati huo huo, vyanzo vya haki za binadamu vilitangaza kuhamishwa kwa watu 100,000 katika siku chache zilizopita na kutangaza kuwa haiwezekani kufikia 64% ya makazi ya Gaza na hakuna mahali salama katika eneo hili.
Your Comment