Kwa kutoa taarifa rasmi, Hezbollah ya Lebanon imekanusha uhusiano wowote na operesheni hiyo ya makombora leo asubuhi (Jumamosi) dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa, madai ya adui yanalenga kutoa visingizio vya kuendelea na uvamizi.
Watu 2 wameuawa Shahidi na watu 10 wamejeruhiwa kutokana na mvutano uliozuka tena Kusini mwa Lebanon na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika eneo la Tolin.