Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, katika hotuba yake ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Shahada ya Muhammad Afif Al-Nablsi na wenzake, alisema: “Haj Muhammad Afif alikuwa na kalamu yenye nguvu katika uandishi na hotuba, na alikuwa na hazina kubwa ya elimu, uelewa mpana, mtazamo sahihi na msimamo ulionyooka.”
Aliendelea kusema kuwa: “Afif kwa zaidi ya miaka kumi alisimamia Idara ya Mawasiliano ya Habari chini ya usimamizi wa Bwana wa Mashahidi wa Ummah, Sayyid Hassan Nasrallah (Allah amwie radhi). Baada ya kuuawa shahidi kwa kiongozi huyo, Afif ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupendekeza kuanzishwa kwa mikutano ya mara kwa mara na waandishi wa habari.”
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah alisisitiza kuwa: “Haj Muhammad Afif alikuwa mwanahabari mwaminifu na mwenye dhamira; katika uwanja wa Kiislamu, kisiasa, na katika njia ya muqawama (mapambano ya ukombozi).”
Mwendelezo wa hotuba
Hotuba hii inaendelea, na taarifa kamili zitatumwa baadaye.
Your Comment