17 Novemba 2025 - 20:59
Mahakama ya Juu ya Iraq yavunja Bunge / Hadi kuundwa kwa Baraza jipya la Mawaziri, Serikali itakuwa tu ya “kusimamia mambo ya kila siku”

Mahakama Kuu ya Shirikisho ya Iraq imetangaza rasmi kumalizika kwa muhula wa tano wa Bunge la nchi hiyo, na kuitaja serikali ya sasa kuwa ni “serikali ya kusimamia mambo ya kila siku”, yenye mamlaka tu katika kushughulikia masuala ya kawaida na yasiyoweza kuahirishwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA- na kwa mujibu wa Kifungu cha 56 cha Katiba ya Iraq, Mahakama Kuu ya Iraq imetangaza kuwa muda wa kisheria wa Bunge umefikia kikomo na kuanzia leo chombo hicho hakina uhalali wa kikatiba.

Katika uamuzi huo imeelezwa kuwa serikali ya sasa, hadi serikali mpya itakapoundwa, itatambulika tu kama “serikali ya kusimamia mambo ya kila siku (caretaker government)”, yenye mamlaka katika kutekeleza tu majukumu ya kawaida yasiyoweza kuahirishwa, kama huduma za kila siku na masuala ya kiutawala.

Mahakama Kuu pia imeonya kuwa serikali haina tena haki ya kuingia katika maeneo makubwa ya maamuzi kama vile kusaini mikataba ya kimataifa, kufanya uteuzi au uteuaji wa watumishi wa juu, kufanya mabadiliko ya kimuundo, au kupitisha sheria nyeti.

Tafsiri hii ya kisheria imetolewa kufuatia ombi la Abdul Latif Rashid, Rais wa Iraq.

Mahakama imesisitiza kuwa Rais ataendelea na majukumu yake hadi baada ya uchaguzi wa Bunge jipya kufanyika.

Kikao cha leo cha Mahakama Kuu ya Shirikisho kimefanyika chini ya uenyekiti wa Mundhar Ibrahim Hussein pamoja na wajumbe wengine.

Katika kikao hicho ilithibitishwa kuwa muda wa kila muhula wa Bunge ni miaka minne kamili, unaoanza katika kikao cha kwanza na kumalizika mwishoni mwa mwaka wa nne.

Mahakama ya Juu ya Iraq yavunja Bunge / Hadi kuundwa kwa Baraza jipya la Mawaziri, Serikali itakuwa tu ya “kusimamia mambo ya kila siku”

Mahakama ya Juu ya Iraq yavunja Bunge / Hadi kuundwa kwa Baraza jipya la Mawaziri, Serikali itakuwa tu ya “kusimamia mambo ya kila siku”

Mahakama ya Juu ya Iraq yavunja Bunge / Hadi kuundwa kwa Baraza jipya la Mawaziri, Serikali itakuwa tu ya “kusimamia mambo ya kila siku”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha