Uongozi wa Chuo cha Al-Mustafa umepongeza matokeo hayo na kusisitiza kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga nidhamu, ukakamavu, maadili na afya ya Mwanafunzi. Uongozi umesema kwamba mafanikio haya ni ushahidi kwamba taasisi za kielimu za Kiislamu zina uwezo wa kutoa mabingwa katika nyanja mbalimbali, si tu elimu na utafiti bali pia michezo na utamaduni.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Chuo cha Kidini cha Al-Mustafa International Foundation – Dar-es-salaam, Tanzania, chini ya usimamizi wa Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) Tanzania, kimeendelea kuthibitisha kwamba Uislamu ni dini inayokuza elimu, maadili, afya na ustawi wa kijamii. Mbali na mafanikio ya kielimu, chuo hicho kimekuwa mstari wa mbele kuhamasisha michezo kama sehemu ya malezi ya mwanafunzi, kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Kiislamu yanayoenzi afya ya mwili na roho.

Katika muktadha huo, wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (saww) walishiriki mashindano ya mchezo wa kitamaduni na kishujaa wa Zurkhaneh, (ambao ni maarufu mno katika nchi za bara la Asia kama vile Iran na India n.k), na unaoendelea kupata umaarufu duniani. Mashindano hayo yalifanyika katika Kitengo cha Utamaduni cha Iran jijini Dar es Salaam yakihusisha timu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki na Kati.

Katika ushindani huo mkali, wanafunzi wa Al-Mustafa waliibuka washindi, na kuwaacha nyuma wapinzani wao kutoka mataifa kadhaa ya eneo hilo la Afrika Mashariki na Kati. Ushindi huo uliwapa heshima ya kipekee ya kuunda rasmi Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Zurkhaneh.

Kutokana na matokeo hayo, Wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) Tanzania sasa wamechaguliwa kuunda Timu hiyo ya Taifa na kuwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Zurkhaneh yatakayofanyika hivi karibuni nchini India.

Your Comment