Donald Trump amesema tena kuwa vita dhidi ya Iran vitamalizika hivi karibuni, akisisitiza kwamba Iran haitawahi kupata silaha za nyuklia na kwamba bei za nishati zitashuka kwa kiwango kikubwa baada ya vita kumalizika.
Mahakama Kuu ya Shirikisho ya Iraq imetangaza rasmi kumalizika kwa muhula wa tano wa Bunge la nchi hiyo, na kuitaja serikali ya sasa kuwa ni “serikali ya kusimamia mambo ya kila siku”, yenye mamlaka tu katika kushughulikia masuala ya kawaida na yasiyoweza kuahirishwa.